ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, January 29, 2015

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA UTUMIAJI WA SIMBANKING NA FAHARI HUDUMA WAKALA


Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.
BENKI ya CRDB imezindua kampeni maalum ya utumiaji wa huduma zake kupitia simu za mkononi 'SimBanking' kupitia kwa mawakala wa 'FahariHuduma'.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama 'Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo', Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei alisema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwakumbusha wateja wake na watanzania wote kwa ujumla umuhimu wa kutumia njia hizo mbadala ili kupata huduma kwa urahisi na uharaka.
Alisema kampeni hiyo inatarajiwa kutoa magari kumi na mbili ambapo kila mwezi mshindi mmoja atazawadiwa gari hilo, pamoja na zawadi ya gari la wateja watakaotumia huduma hizo pia wataweza kujishindia zawadi nyingine mbalimbali zikiwemo solar power, tables na simu za kisasa za mkononi.
"Tunataka kuwavutia wateja wetu kuziamini na kuzitumia zaidi huduma hizi kwani ni sawa kabisa na kupata huduma kupitia matawi yetu,".
 
 
 
Akielezea namna ya kushiriki na jinsi mshindi atakavyopatikana, Dk. Kimei alisema kuwa shindano hilo ni la wateja wote wa CRDB watumiao huduma hizo na mshindi atakuwa ni yule mwenye miamala mingi zaidi kwa mwezi husika.
"Mshindi ni yule atakayekuwa amefanya miamala mingi zaidi kwa kutumia SimBanking au FahariHuduma katika mwezi husika, iwe ni kutumia fedha kwenda kwenye akaunti nyingine, au kwenda kwenye mitandao ya simu au kulipia Ankara," alisema.
Kwa upande wake ,Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Martin Mmari alisema ubunifu ndio njia pekee itakayotatua changamoto, ni muda muafaka kwa Watanzania kuchangamkia fursa hiyo na kujishindia zawadi.

Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kuzungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi 'SimBanking', kupitia kwa mawakala wa 'FahariHuduma', ijulikanayo kama 'Tuma pesa na SimBanking shinda Passo' uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati) akiwa na maofisa wa benki hiyo.

Maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.

Maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi 'SimBanking', kupitia kwa mawakala wa 'FahariHuduma', ijulikanayo kama 'Tuma pesa na simBanking shinda Passo'

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...