Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba.
Tume
ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau
wengine wote kuwa Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe.
Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 katika Viwanja
vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Hafla
hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya
siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.
Taarifa zaidi kuhusu hafla hii zitatolewa baadaye.
No comments:
Post a Comment