
Messi akipokea tuzo yake

Messi akishangilia moja ya mabao yake

Messi akishikilia kikombe cha ushindi

Messi akipongezwa na baadhi ya mashabiki
Mshambulizi
wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ameshinda tuzo
ya Ballon d’Or kwa mwaka wa nne mfululizo. Messi, 25, alifunga jumla ya
magoli 91 mwaka wa 2012 na aliwashinda wachezaji wengine Andres Iniesta
wa Barcelona na Christiano Ronaldo wa Real Madrid.
Messi
alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu walioteuliwa na jopo la wandishi
wa habari na makocha wa timu za taifa, manaodha wa timu hiyo wakiwa ni
pamoja na Iniesta na Ronaldo.
Messi
alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo ya the Ballon d’Or, tuzo ambayo
hukabithiwa mchezaji bora wa mwaka katika sherehe iliyofanyika mjini
Zurich
Kwasasa
Mesi ni mchezaji wa kwanza kuwahi kushinda tuzo hiyo ya Ballons d’Or,
kwa miaka minne mfululizo, rekodi anayoshikilia na aliyekuwa mchezaji wa
Ufaransa na rais wa UEFA kwa sasa Michel Platini.
Abby Wambach, alishinda tuzo kwa upande wa kina dada naye Vicente del Bosque, akituzwa kuwa kocha bora.
No comments:
Post a Comment