Pichani
Juu na Chini ni Lundo la matawi ya miti yanayodaiwa kukatwa na Shirika
la Umeme Tanesco nakuachwa chini ya kizagaa hovyo bila kujulikana
utaratibu wa kuyazoa. Eneo hili ni karibu na Hotel ya Southern Sun
kuelekea jengo la Pam Residence maeneo ya Ocean road jijini Dar.
Lundo la matawi ya miti lilotelekezwa na Tanesco katika maeneo ya karibu na ofisi za Shirika la Afya duniani WHO.
Hapa ni ukuta wa Chuo cha usimamizi wa fedha IFM.
Afisa
Habari wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Vidah Fammie
akizungumzia changamoto kampuni hiyo inayokumbana nazo wakati wa
kutekelezaji wajibu wao wa kufanya usafi na kutolea mfano kubwa likiwa
la matawi ya miti kuachwa hovyo barabarani.
Amesema
Kampuni yake inashughulika na Domestic Garbage lakini swala la miti
liko nje ya kazi za kampuni hiyo na kuashauri kuwa ingekuwa vizuri mtu
anapotaka kukata miti awasiliane nao waweze kushauriana juu ya uzoaji wa
taka hizo.
Amesema
taka za aina hiyo zinazongeza gharama kwa kampuni ya Green Waste Pro
Ltd kwa kuwa magari yake ni maalum kwa ajili ya kubeba Domestic Garbage
hivyo yoyote atakayetaka kufanya zoezi la kukata matawi ya miti
pembezoni mwa barabara za jiji anapaswa kutoa taarifa mapema.
Kampuni
ya Green Waste Pro Ltd imekuwa ikilishitumu shirika la Umeme Tanesco
kwa kukata matawi ya miti na kuyaacha yakizagaa katika barabara na kuwa
hiyo si mara ya kwanza shirika hilo limekuwa likifanya hivyo mara
kadhaa, kwani kipindi cha nyuma waliwahi kuacha matawi barabarani na
kampuni hiyo ikawajibika kuingia gharama ya kuzoa taka hizo na
ilipowaandikia Invoice ya kwamba wamechafua mji na kampuni hiyo
imechukua jukumu la kufanya usafi hivyo inawadai walikaidi kulipa.
Leo
kampuni hiyo imeendelea na zoezi la kukata matawi ya miti na kuyaacha
katika barabara tofauti za jiji yakizagaa hovyo huku haijulikani nani
anawajibika kwenda kuzoa.
No comments:
Post a Comment