Waziri wa mambo ya ndani emmanuel Nchimbi afungua Mafunzo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk.
Emmanuel Nchimbi (kulia) akipokelewa na Kamishna wa Sheria na Utawala wa
Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa kabla ya kufungua mafunzo ya Jinsia
kwa wakuu wa magereza wa mikoa yote Tanzania Bara, maafisa waandamizi wa
makao makuu, watumishi raia na askari kutoka magereza mbalimbali
nchini. Mfunzo hayo ya siku nne yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Edema mjini Morogoro.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ili afungue
mafunzo ya jinsia kwa maafisa magereza nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi akizungumza na maafisa mbalimbali wa jeshi la magereza
kabla ya kufungua mafunzo ya jinsia kwa maafisa hao. Kushoto ni Mkuu wa
Jeshi la Magereza nchini, John Minja na Kamishna wa Huduma za
Urekebishaji wa Jeshi hilo, Deonis Chamulesile.
Maafisa Magereza wakimsikiliza kwa
makini Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (hayupo
pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya
jinsia.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi (kulia) akimshukuru Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa
Programu ya Mabadiliko ya Sekta ya Sheria nchini, Bi. Wanyenda Kutta
baada ya kumkabidhi taarifa ya hali ya Utekelezaji wa Masuala ya Jinsia
katika Taasisi zinazotekeleza Programu ya Maboresho ya Sekta hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi (wa katikati waliokaa) akiwa na Wakuu wa Magereza ya
Mikoa yote ya Tanzania Bara katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment