

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba.
DODOMA.
WAZIRI
wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe ameingia katika msuguano wa
chinichini na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu,
Peter Serukamba ambaye alidaiwa kuongeza maneno kwenye hotuba ya kamati
yake yaliyokuwa yakimlenga waziri huyo binafsi.
Kutokana
na hali hiyo, hotuba iliyokuwa isomwe na Serukamba kama maoni ya kamati
baada ya Dk Mwakyembe kuwasilisha hotuba yake, ilibadilishwa dakika za
mwisho na kusainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Juma
Kapuya.
Mmoja
wa wajumbe wa kamati hiyo (ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe)
alisema waliamua kuunda kamati ndogo ya wabunge wanne kusahihisha lugha
iliyotumika katika kuandaa maoni ya kamati hiyo kuhusu Hotuba ya Bajeti
ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014.
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, wajumbe waligundua kuwa lugha iliyotumika
ililenga kushambulia moja kwa moja Dk Mwakyembe ndani ya Bunge jambo
ambalo lilk
uwa kinyume cha makubaliano ya kamati.
Hata
hivyo, Serukamba akizungumza na gazeti hili alikana kubadili hotuba
hiyo na kuongeza kuwa; “Mimi nimerudi jana, kwa kawaida kamati
ikishajadili suala la hotuba kuandikwa tunamwachia Katibu na akimaliza
anairudisha kwetu wabunge.
Hivyo nilichokisoma ndicho tulichokubalina na wajumbe wa kamati hiyo.”
Aliongeza:
“Msitake kunigombanisha na mheshimiwa Waziri, mimi ndiyo kwanza
nimeingia asubuhi hii hakuna kilichobadilika katika hotuba hiyo.”
Gazeti
hili lilifanikiwa kuona nakala mbili za hotuba za kamati, moja ikiwa na
saini ya Serukamba na nyingine ikiwa imesainiwa na Profesa Kapuya na
zote zina tarehe inayofanana ambayo ni Mei 16, 2013.
Kwa
upande wake Kapuya katika majibu ya maandishi kwa gazeti hili alisema si
kweli kwamba ziliandikwa hotuba mbili. “Habari hizo hazina ukweli,
kamati yangu ina utaratibu wa kuandaa hotuba yetu na ikishakamilika
tunateua kamati ndogo ambayo inapitia hotuba hiyo kabla ya
kuisoma,”alisisitiza Profesa Kapuya.
Majibu ya
Serukamba na Kapuya yanatofautiana na kauli ya Dk Mwakyembe ambaye
aliliambia gazeti hili kwamba pia alipata taarifa za kuwapo kwa mpango
huo kutoka kwa “watu wanaojua na kuthamini kazi yake.”
“Siyo
kila mtu anaweza kukuchukia huwezi kunyimwa maneno, watu wenye imani na
mimi walikuja kunipa taarifa na wakanipatia ile aliyokuwa ameandika
yeye…. ana bahati sana nilikuwa namsubiri kwa hamu aisome hiyo hotuba
yake nilipanga kumchanachana pale pale asingeamini,”alisisitiza Dk
Mwakyembe.
Alipoulizwa
kwa nini anafikiri mwenyekiti huyo ameamua kumfanyia hivyo, Dk
Mwakyembe alisema; “Siwezi kujua lakini naamini hizi ni mbio tu za mwaka
2015.”
Naibu
Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema hafahamu kuhusu suala hilo.
“Ninachofahamu ni kwamba Serukamba alikuwa amesafiri kwenda China na
mimi nilimwona siku hiyo akisoma maoni ya kamati yake, kama kulikuwa na
tatizo hilo pengine litakuja baadaye ofisini kwetu,”alisema Ndugai kwa
simu.
Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/2013/05/waziri-dk-mwakyembe-serukamba-wavutana.html#ixzz2TcuDbFxz
No comments:
Post a Comment