Mshindi wa kombe la dunia na mchezaji bora wa dunia wa zamani mbrazil Rivaldo ametengeneza historia mpya katika soka.
Mshambuliaji wa zamani wa FC Barcelona ameweka historia ya
kucheza pamoja na mwanae wa kiume katika timu moja ndani ya uwanja ambao
umepewa jina lake huko nchini Brazil.
Rivaldo, 41, aliingia kama mbadala kwa timu ya Mogi Mirim
wakati walipotoka sare ya 1-1 dhidi ya timu ya XV de Piracicaba katika
ligi ya mji wa Sao Paolo.
Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa baba na mtoto kucheza pamoja
tangu Rivaldo mkubwa aliporejea nyumbani Brazil akitokea nchini Angola
alipokuwa anaichezea klab ya Kabuscorp.
Mtoto wa Rivaldo ana miaka 18, ana kazi kubwa ya kufuata nyayo za baba yake na kuhakikisha anafika alipofika mzazi wake.
No comments:
Post a Comment