STAA wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amekiri kubebeshwa
madawa ya kulevya bila kujua na kujikuta akiponea chupuchupu kutokana na
umaarufu wake.
Akizungumza na paparazi wetu, Dude alisema amewahi kubebeshwa unga na rafiki yake wa karibu ambaye hakumtaja jina na
walikuwa wakitokea Nairobi nchini Kenya kuja
Tanzania.Alisema wakati wanaanza safari alipewa koti la baridi na rafiki
yake huyo, akalivaa kumbe ndani yake lilikuwa limeshonewa pakti za
unga.
Walisafiri kwa gari na kila walipokutana na polisi wanaokagua
hawakumkagua Dude kwani waliishia kupiga naye picha na kumsifia kwa kazi
yake mpaka alipofika jijini Dar es Salaam.
“Kila tulipokuwa tunakutana na polisi rafiki yangu alikuwa akiwawahi na
kuwaambia kwamba yupo na mimi ambapo walifurahia kuniona na kupiga picha
na mimi bila kunikagua chochote,” alisema
Dude.
Dude.
Baada ya kupita vizingiti vyote, waliingia jijini Dar es Salaam maeneo
ya Kinondoni Manyanya alipokuwa akiishi rafiki yake huyo ambapo
alimwambia avue koti, akaanza kufungua mzigo aliokuwa ameushonea kwa
ndani.
Dude alijikuta akishikwa na tumbo la kuhara kutokana na mshtuko
alioupata baada ya kuona rafiki yake huyo akitoa madawa ya kulevya.
“Jamaa alinipa shilingi elfu hamsini za Kenya na ni baada ya kufika Dar
ndipo niligundua kwamba nilikuwa nimebebeshwa unga lakini yule jamaa
alishakamatwa na anatumikia kifungo nchini Pakistani,” alisema Dude.
Hata hivyo Dude aliwashauri mastaa wenzake kuwa makini na marafiki zao
kwani siyo wote wanaokamatwa wamebeba unga kwa kujua bali wengine
wanabebeshwa tu bila kujua.
No comments:
Post a Comment