Msanii
wa Bongo Movie, Rachel Haule ‘Recho’ (pichani), amefariki dunia usiku
wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
slaaam. Habari zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve
Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo
mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya,
ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki
dunia.
Source: EATV Facebook Page
Source: EATV Facebook Page
No comments:
Post a Comment