ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, May 15, 2014

Yanga yazidiwa na Simba


 
Abdi banda akimwaga wino Coatal Union mwaka jana june 18

YANGA ilikuwa katika mchakato wa kumsajili beki wa kushoto wa Coastal Union, Abdi Banda, lakini Simba imeingilia kati na imebakiza asilimia ndogo tu kumsainisha mkataba na hata mchezaji mwenyewe ameshanogewa na Msimbazi.
Yanga ndio walioanza kuzungumza na beki huyo mrefu ambapo jopo la usajili pamoja na baadhi ya watu wa ufundi walitaka asajiliwe haraka na wakajenga hoja kwa kocha, Hans Pluijm, lakini akawakatalia kwa hoja.
Pluijm ambaye amemaliza mkataba Yanga aliwaeleza kwamba Banda hana kasi inayotakiwa katika beki wa kushoto na hivyo haafiki yeye kusajiliwa Yanga, hivyo Yanga wakatulia lakini bado kuna wajumbe walikuwa hawajaridhika na walitaka kumshawishi Kocha Msaidizi, Boniface Mkwasa juu ya mchezaji huyo.
Hata hivyo bado wakiwa wanajivutavuta, Simba ikamnyaka na kufanya naye mazungumzo haraka na sasa wako katika mchakato wa kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja Coastal.
Kumsainisha mchezaji huyo kunamaanisha kwamba kutakuwa vita ya kugombea namba na baina yake na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
Mmoja wa mabosi wa Simba ameliambia Mwanaspoti kwamba kila kitu kimeshakamilika katika kumchukua beki huyo ambapo jambo la kwanza ni kuvunja mkataba wake na Coastal.
Hivyo wapo katika mazungumzo ya karibu zaidi na uongozi wa Coastal na yanachelewa kukamilika kutokana na mgawanyiko ulioko ndani ya uongozi wa timu hiyo ya jijini Tanga.
“Hata huu uchaguzi ndiyo unatuchelewesha, lakini vinginevyo tungeshamsainisha haraka, tunamhitaji sana yule kijana,” alisema bosi huyo.
Kufuatia taarifa hizo Mwanaspoti lilimtafuta Banda ambaye alikiri kufikia makubaliano ya kila kitu na Simba ambapo alisema wakati wowote anaweza kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.
“Nikweli nimezungumza na Simba kifupi ni kwamba tumeshakubaliana kila kitu kuhusu mambo muhimu, tumebakiza kitu kimoja tu kumalizia kwa kusaini lilikuwa suala la kuvunja mkataba na Coastal,” alisema Banda.
Mchambuzi wa soka, Edo Kumwembe, akimzungumzia mchezaji huyo alisema: “Banda anajiamini, kweli hana kasi na ni mchezaji mbunifu, lakini kocha atakayemsajili inabidi afanye kazi ili kuziba tatizo lake la kutokuwa na kasi.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...