Bendera ya Jumuia ya Afrika Mashariki
Marais wa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana leo mjini
Nairobi, Kenya baada ya kutofanyika mkutano wa awali uliokuwa umepangwa
kufanyika mwezi wa Desemba mwaka jana mjini Nairobi.
Marais wote watano wa nchi wanachama wanatarajiwa kuhudhuria.
Katika
mkutano huo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania anatarajiwa kukabidhiwa
Uenyekiti wa Jumuia hiyo kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya,
wadhifa ambao alikuwa akabidhiwe mwezi Desemba mwaka jana, lakini
hakuweza kuhudhuria mkutano huo kutokana na kwenda kutibiwa nchini
Marekani.
Rais
Jakaya Kikwete wa TanzaniaMarais wote watano wa nchi wanachama wa Jumuia
ya Afrika Mashariki, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda,
Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Jakaya Kikwete wa Tanzania na mwenyeji wa
mkutano Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Mbali na
masuala ya uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii miongoni mwa mataifa
hayo, kujadiliwa katika kikaohicho, pia maombi ya nchi za Sudan Kusini
na Somalia kuomba uanachama wa jumuia ya Afrika Mashariki yatajadiliwa.CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment