
MWANASOKA
bora wa Dunia Cristiano Ronaldo alipewa kadi nyekundu ya utata wakati
Real Madrid pungufu ya mchezaji mmoa ikilazimishwa sare ya 1-1 na
Athletic Bilbao jana Uwanja wa San Mames katika La Liga.
Mshambuliaji huyo alitolewa nje baada ya kumuwakia Carlos Gurpegi na baadaye kugombana na Ander Iturraspe dakika ya 75.
Dakika
moja kabla, Athletic walipata bao la kusawazisha lililofungwa na Gomez
aliyetokea benchi kufuatia Jesse kuifungia Real bao la kuongoza dakika
ya 65.
Matokeo
hayo yanaifanya Real itimize pointi 54 na kubaki nafasi ya tatu katika
msimamo wa La Liga, baada ya kucheza mechi 22, nyuma ya Barcelona yenye
pointi 54 pia.
Ushindi
wa maba 4-0 wa Atletico Madrid jana dhidi ya Real Sociedad unawapandisha
kileleni baada ya kutimiza pointi 57 katika mechi 22 pia. Shukrani kwao
David Villa, Diego Costa, Miranda na Diego waliofunga mabao hayo Uwanja
wa Vicente Calderon. chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment