KAMA YESU ALIVYOSEMA WATAKUJA MANABII WENGI WAKIJIFANYA WAO NDO KRISTO,HUYU NDIO KRISTO FEKI ANAYE TIKISA DUNIA KWA SASA
SHETANI bado anazidi kuwasakama Wakristo duniani. Hii ni baada ya mkazi wa Kijiji cha Alvaro Thesiss, Santa Catarina nchini Brazil, Mtume Inri Cristo (66) mwanzilishi wa Kanisa la Waraka Mweusi (Suprema Ordem Universal da SantÃssima Trindade ‘Soust’), miaka 35 iliyopita kujitangaza kuwa yeye ni Yesu Kristo amerudi kuja kuwaokoa wanadamu baada ya kusubiriwa kwa miaka mingi.
Mtume Inri Cristo 'Yesu feki' akifanya maombi pembeni ni wafuasi wake.
Cristo kwa sasa anaitikisa dunia kwa kuwahubiria maelfu ya watu wa madhehebu ya Kikristo sehemu mbalimbali duniani huku akijiita Yesu Kristo wa Nazareti.
MAHUBIRI YAKE YATIKISA
Mei, 2013, Cristo alitua katika Jiji la Sao Paulo nchini humo na kuwaombea Wakristo, wakiwemo makahaba. Alipokelewa kwa heshima zote huku akijitangaza kuwa hakuna atayekuja duniani kuwakomboa wanadamu zaidi yake.
Mtume Inri Cristo 'Yesu feki' akimuombea muumini.
Alihubiri kuwa kwa kila kiumbe mwenye matarajio ya kuingia kwenye ufalme wa mbinguni yeye ndiye njia ya kweli na uzima.
YESU FEKI AKUTANA NA MAGUMU
Septemba,
2013, mzee huyo alitua kwenye Jiji la Rio de Jeneiro kwa lengo hilohilo
lakini alijikuta akishambuliwa vikali huku Wakristo wa jiji hilo
wakimtupia lawama kuwa ni mhubiri feki aliyevaa ngozi ya kondoo
kujipatia kipato kinyume na utaratibu wa makanisa mengine ya Kikristo
nchini Brazil.
AITWA MHUBIRI PUNDA
Akiwa
katika harakati zake za kuwavuta waumini wa makanisa ya Kikristo katika
Jiji ya Sao Paulo wakati wa Sikukuu ya Krismasi, mwaka jana, mhubiri
huyo feki alishambuliwa tena na waumini wa eneo hilo ambao walikusanyika
kwenye mkesha wa sikukuu hiyo.

Yesu feki akiwa kwenye kiti chake.
Baadhi
ya waumini walimzomea kwa mahubiri yake huku wakisema hayana tofauti na
punda aliyebebeshwa mzigo mzito na kushindwa kuutua.
Hata hivyo,
Yesu feki huyo aliwajibu waumini hao kwamba hawajui walitendalo kwani
yeye ndiye Yesu wa kweli aliyetumwa na Mungu kuja duniani kuwaokoa
wanadamu.
“Mimi sijali maneno yao, wameniita punda, eti mahubiri
yangu hayana tofauti na punda aliyebebeshwa mzigo mzito hivyo hawezi
kujinasua siku zote ataishia kutapatapa, mimi nimetumwa na Mungu,”
alisema Cristo.

ANASWA NA KASHFA YA UTAPELI
Akiwa
amejiamini na kujijengea heshima kubwa kwa waumini wake, Januari Mosi
mwaka huu, mhubiri huyo alishambuliwa kwa maneno na watu wasiojulikana
kwa kusambaza nyaraka za wazi zilizokuwa zimeandikwa kuwa yeye ni tapeli
mkubwa kwani anadanganya watu ili kujipatia fedha.
Kitendo
hicho kilimpunguzia umaarufu kwani alikuwa ameweka utaratibu kwa
waumini wake kulipa fungu la kumi kwa kila pato, alijiweka zaidi kwa
wafanyabiashara wakubwa nchini Brazil huku akiwaonya kuwa bila yeye
hawawezi kufanikiwa kimaisha.
HISTORIA YAKE KIDUNIA
Cristo
aliyezaliwa Machi 22, 1948 mwenye wafuasi wengi katika kanisa lake,
amewahi kutembelea nchi nyingi duniani akieneza uzushi huo kwamba yeye
ni Yesu Kristo.

Yesu feki akiomba.
Amewahi
kufukuzwa kwenye baadhi ya nchi za Ulaya na Amerika ya Kusini zikiwemo
Uingereza, Venezuela, Peru, Marekani na Ufaransa ambako alitaka
kuanzisha makanisa. Pia ameshawahi kuwekwa ndani mara 40 nchini mwake
kutokana na kujitangaza kuwa yeye ni Yesu na kuvuta watu wengi.
Katika
nchi yake, Cristo amefanikiwa kuwafanya waumini wake waishi pamoja naye
kwenye makazi jirani na kanisa lake la Santa Catarina.
Wazazi wa mzee huyo, baba Wilhelm na mama Magdalena Thais ni Wakatoliki wenye asili ya nchini Ujerumani.
Tangu
mwaka 1979, Cristo amesafiri zaidi ya nchi 27 duniani kote akieneza
neno lake huku akisema yeye ni Mfalme wa Wayahudi aliyerejea duniani kwa
mara ya pili. Pia husema eneo la kanisa lake ni Yerusalemu mpya.

...Akiwaombea waumini.
MAVAZI YAKE
Mara
zote, Cristo huvaa kanzu nyeupe na viatu vya ‘makubazi’ huku kichwani
akiwa na mduara wenye kuashiria taji la miiba alilovalishwa Yesu wa
kweli.
ETI ALIISIKIA SAUTI YA MUNGU
Katika
mahojiano yake na baadhi ya redio nchini humo, mhubiri huyo amekuwa
akisema tangu utotoni mwake alikuwa akiifuata sauti ya Mungu ambayo
ilikuwa ikisema: “Mimi ni Baba yako. Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo.”
ANA MPANGO WA KUTEMBELEA AFRIKA
Inasemekana wakati wowote mwaka huu, Cristo atatembelea nchi mbalimbali za Bara la Afrika kwa lengo la kuvuta wafuasi wengi.
Nchi
za Zimbabwe, Afrika Kusini, Tanzania, Togo, Mali, Misri, Angola,
Nigeria, Burkina Faso na Zaire zinadaiwa kuwepo kwenye ratiba ya ‘Yesu’
huyo.
VIONGOZI WA DINI NCHINI WAMKEMEA
Gazeti hili lilizungumza na baadhi ya wachungaji na maaskofu wa Tanzania kusikia wanamzungumziaje mhubiri huyo feki.

MCHUNGAJI MTIKILA
Mchungaji
wa Kanisa la Full Salvation Church la jijini Dar es Salaam, Christopher
Mtikila alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusiana na sakata hilo, alisema:
“Huyo ni shetani mkubwa, akija Tanzania hatutaki kumwona kwani anakuja kuwavuruga waumini wetu.”

ZAKARIA KAKOBE
No comments:
Post a Comment