Mwenyekiti
wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wanachama wa
chama hicho wa mkoa wa Dar es salaam waliomwandalia hafla ya kumpongeza
jana Novemba 18, 2012 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.(PICHA
NA IKULU).
Na Mwandishi wa Thehabari.com
Sekretarieti
mpya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyoingia madarakani hivi karibuni
chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, imesema itahakikisha vitendo
vya rushwa hasa kwenye chaguzi za chama hicho vinakoma mara moja,
tofauti na ilivyokuwa imezoeleka.
Kauli
hiyo ya viongozi wa juu wa CCM, Mwenyekiti Taifa (Rais Kikwete), Makamu
Mwenyekiti Tanzania Bara (Phillip Mangula) na Katibu Mkuu (Abdulrahman
Kinana) imetolewa jana na viongozi hao wakati wakizungumza na wana-CCM
Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano wa kumpongeza Rais Kikwete
kuchaguliwa kushika nafasi hiyo tena.
Akizungumza
na umati wa wanachama hao, Rais Kikwete aliwataka viongozi wapya
kufanya kazi ya ziada ya kuhakikisha wanarejesha imani ya Watanzania kwa
CCM, ambayo haiko kama ilivyokuwa zamani.
“Lazima
kujiuliza nini kimekifanya chama hiki kufikia hapo kilipo na kuangalia
nini cha kufanya ili kuondokana na hali hiyo. Pale mnapohisi hali ya
kuungwa mkono inapungua lazima tujiulize, kulikoni..! Nini cha kufanya
ili kuimarisha chama,” alisema na kuongeza kuwa kazi nyingine ni
kuhakikisha wanakijenga chama na kuimarisha zaidi ili kiendelee
kuwaongoza Watanzania.
“Chama
chetu hakifanyi mikutano…wenzetu wanafanya kwanini sisi hatufanyi, sasa
tutatengeneza utaratibu maalumu kuhakikisha viongozi wa chama kwa
nafasi zao wanafanya kazi yao ipasavyo ndani na nje ya chama,” alisema
Rais Kikwete.
Alisema
ipo haja ya kujipanga na kuangalia namna ya kupambana na propaganda
hasi za baadhi ya vyombo vya habari na wapinzani ili kukabiliana na hali
hiyo. Aliwataka wanaCCM kuacha makundi na chuki ambayo yamekuwa
yakikigawa chama hicho.
Awali
akizungumza Kinana alisema vitendo vya rushwa ndani ya CCM
watahakikisha vinakoma mara moja ili kurejesha imani ya Watanzania
iliyopungua kutokana na tuhuma za wachache dhidi ya vitendo viovu.
Alisema
chini ya uongozi wake atahakikisha mashaka yaliotawala kwa wananchi
dhidi ya CCM yanaondoka kwa kuwaengua wale wanaoendeleza vitendo vya
rushwa, majumbu na vitendo vinavyo leta sifa mbaya ya chama hicho.
“Hatuwezi
kuiongoza nchi yetu wakati watu wanamashaka na sisi, lazima tuondoe
mashaka akisimama mwana-CCM wote waseme naam huyu anaweza kusema…sio
akisimama mwana-CCM kusema watu wanahoji haaah, na huyu naye anakemea
rushwa?
Aliwataka
wana-CCM kushirikiana katika kukisafisha chama na si kuwaachia viongozi
jukumu hilo, ambalo wao kama viongozi wamekubali kuongoza mapambano
hayo.
Alisema
CCM ina wanachama milioni 5 ambao asilimia 99.9 wengi wakiwa ni
masikini na waadilifu huku asilimia 0.1 wakiwa ni wala rushwa wakubwa,
wapenda mizengwe, wapendeleaji hivyo kujikuta idadi hiyo ikikichafua
chama chote jambo ambalo alisema chini ya uongozi wao hawawezi kuacha
hali hiyo iendelee.
Alisema
atahakikisha anasimamia ilani ya chama vizuri huku kanuni mbalimbali
zikifuatwa ili kuleta haki ndani ya chama hicho, alisema kuna kazi kubwa
ya kukijenga chama hicho,
Alisema
pamoja na viongozi wenzake watahakikisha baadhi ya wana-CCM waliokuwa
na tabia za mizengwe pamoja na kupanga safu za viongoli ili kubebana
kimaslahi inatoweka, hivyo kumtaka kila mwanachama afanye kazi ya
kumuingizia kipato na si kutegemea kunufaika na nafasi ya uongozi.
Naye
Makamu Mwenyekiti Bara, Mangula alisema wapo baadhi ya viongozi
wameingia ndani ya chama kwa rushwa na tayari malalamiko juu ya mizengwe
ya uchaguzi wa chama hicho uliofanyika yamewafikia, hivyo kwa sasa
wataanza kupitia kwa kina kila malalamiko na atayebainika kuingia kwa
rushwa ataenguliwa bila kumuogopa.
“Tunajipa
miezi sita ndani ya miezi sita walioingia kihalali wataendelea lakini
walioingia hovyo hovyo ‘out’…walioingia kwa pesa nje, hata wale
waliokuwa wanatumwa vibahasha nao tukiwajua wale nje, hatukubali chama
chetu kituhumiwe kwa rushwa, wala hatuta ngoja ushahidi sijui wa
TAKUKURU, Polisi hakuna tutakisafisha Chama Cha Mapinduzi,” alisema.
“…Lakini
na nyingi mliokubali kununuliwa kama sambusa mlifanya makosa,
tusikubali tena…kwanini mtu ukubali kuthaminishwa kama sambusa?,”
-Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment