Rais mpya wa China Xi Jinping
Ingawa mfumo wa uongozi wa taifa la Tanzania ni wa kidemokrasia, tuliokuwa tunafuatilia uchaguzi wa viongozi huko Uchina wakati huo huo tukifuatilia uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi hapa Tanzania, aina hizi za uchaguzi zinafanana kwa kiasi kikubwa sa.
Mwenyekiti wa chama cha Kikomunist cha China ndiye anayekuwa rais moja kwa moja na viongozi wengine wote waandamizi wanafuata kutokana na rank wanazokuwa nazo kwenye chama kuanzia waziri mkuu, naibu waziri mkuu, makamu wa rais na kiongozi wa chama huko Shanghai. Binafsi nilipotembelea Shaghai mwaka 2007 niligundua jinsi jimbo lile lilivyokuwa na nguvu na mara nyingi mtu akichaguliwa kukiongoza chama Shanghai ni kama jaribio la kumfanya kuwa rais na ndivyo ilivyokuwa kwa bwana Xi ambaye mwaka 2007 aliteuliwa kuwa kiongozi wa chama cha kikomusnist cha China huko Shanghai.
Kinachofurahisha zaidi au kinacholeta gumzo kubwa huko Uchina kuanzia asubuhi ya leo ni mke wa rais Bwana Xi aitwaye Peng Liyuan ambaye ni popstar (mwanamuziki) maarufu kuliko wote China kwa sasa. Nitamaliza tafsiri ya mke huyu wa rais na kesho nitaandika makala ya kutosha kuhusu mama huyu maarufu sana katika bara la Asia.
Mke wa rais (First Lady) wa China
Mke wa rais (First Lady) mpya wa China
Hata hivyoo, Bwana Xi Jinpingalikuwa kati ya viongozi waandamizi wa Jehsi la Uchina. Bwana Xi ataongoza Uchina kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia leo tarehe 15/11/2012 hadi 14/11/2022 atakapokuwa na miaka 69.
Akiongea
wakati wa mkutano huo Bwana Xi alisema kuwa, chama hicho kinakabiliwa
na changamoto nyingi lakini atafanya kazi ili kuhakikisha kuwa ameafikia
matakwa na matarajio ya raia wa nchi hiyo.
Wengi wa viongozi wapya katika kamati hiyo
wanaonekana kuwa wanasiasa wahafidina na wale waliokisiwa huenda
wakaleta mabadiliko hawakupandishwa cheo.
Xi Jinping anachukua mahala pa Hu Jintao, ambaye chini ya utawala wake, uchumi wa Uchina umekuwa kwa kiasi kikubwa.Hatua hiyo sasa imekalisha shughuli rasmi ya kukabithi madaraka ya nchi kwa kizazi kipya. Kama ilivyokuwa kwa CCM jana, vijana na sura mpya kabisa zimeibuka katika Secretariate na nec kwa Uchina ni hivyo hivyo. Pamoja na Bwana Xi Jinping ni Zhang
Dejiang, kiongozi wa chama hicho mjini Shangai, Yu Zhengsheng, afisa
mkuu anayehusika na masuala ya habari na propaganda Liu Yushan, Naibu
Waziri Mkuu Wang Qishan na kiongozi wa chama cha Tianjin Zhang Gaoli.
Viongozi hao wana majukumu makubwa na Bwana Xi,
amesema dhamira yao kuu ni kuunganisha na kuongoza chama hicho na
kuifanya taifa hilo kuwa thabiti na lenye ushawishi zaidi. Hata hivyo Baraza la Uongozi wa juu la China limepunguzwa kutoka watu 9 hadi 7 wenye uchawishi mkubwa zaidi nchini humo.
Viongozi saba wenye ushawishi mkubwa zaidi China ambao ndiyo watakaoongoza taifa kubwa la Uchina kwa kipindi cha miaka kumi
Baada ya mkutano huo kukamilika, Bwana Xi,
aliondoka kwenye ukumbi huo akifuatwa na Bwana Li Keqiang, ambaye
atamrithi Waziri mkuu wa nchi hiyo Wen Jiabao, na wanachama wengine
watano wenye ushawishi mkubwa katika kamati hiyo kuu ya chama. Mkutano Mkuu wa Chama cha kikomunist wa China unajulikana kwa jina maarufu kama Politburo. Mabadiliko haya ya uongozi katika Taifa kubwa kiuchumi duniani na TAifa linaloongoza hivi sasa kwa michango yake katika Bara la Afika hususan Tanzania, utakuwa na athati gani kwetu?
Na Richard Bahati
Kama CCM kweli
ReplyDelete