Mke
wa balozi wa Ireland nchini Tanzania (wa kwanza kushoto), Sarah Colins
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika
ubalozi wa Uswisi, kuhusu maonesho ya hisani yatakayonyika siku ya
jumamosi jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili
ya watu wanaoishi katika mazingira magumuna kufunguliwa na mke wa
Makamu wa Rais Bi. Asha Bilal siku ya jumamosi. Pamoja nae ni
Mwenyekiti wa kundi hilo Juliana Parroni (Switzeland) na Keiko Okada
(Japan).
Mwenyekiti
wa kundi la wake wa mabalozi nchini (DSG) Juliana Parroni,(kulia)
akizungumza na waandishi wa habari, juu ya maonyesho ya hisani yatakayo
fanyika siku ya jumamosi na kufunguliwa na Mke wa makamu wa Rais, Bi
Asha Bilal kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa watu wanaoishi katika
mazingira magumu. Kutoka kushoto ni mke wa Balozi wa Namibia Aletha
Aisaack, Sara Colins (Ireland) Keiko Okada (JAPAN) na Kaisa Alapartanen
(Finland).
Mke
wa Balozi wa Japani nchini Tanzania (wa kwanza kutoka kulia) Keiko
Okada, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya
Maonyesho ya hisani yatakayofanyika mwisho wa wiki ili kuchangisha fedha
kwa ajili ya makundi ya watu wasiojiweza, pamoja nae kutoka kushoto ni
Mke wa Balozi waIreland Sarah Colins na katikati ni Mwenyekiti wa umoja
huo Bi. Juliana Paroni. Maonyesho hayo yatafunguliwa na Bi. Asha Bilal
Mke wa makamu wa Rais.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Asha Bilal, anatarajia kuwa Mgeni rasmi katika Maonyesho ya Hisani yaliyoandaliwa na kundi la wake wa Mabalozi nchini. (DSG)
Maonyesho
hayo yatakayo fanyika Novemba 17, mwaka huu katika viwanja vya Shule ya
Kimataifa ya Tanganyika, jijini Dar es Salaam, hufanyika kila Mwaka kwa
ajili ya kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii zenye mahitaji
maalumu hasa wanawake, watoto na walemavu wanaoishi katika mazingira
magumu ikiwa ni mala ya pili Mke wa Makamu wa Rais kuendesha
uchangishaji huo.
Mwaka 2011,
Umoja huo kupitia maonyesho ya hisani ulikusanya jumla ya Shilingi
milioni 73, ambazo zilisambazwa kama ufadhili kwenye miradi 15 ya hisani
na taasisi binafsi Tanzania Bara na Visiwani, michango hiyo hufikia
shilingi milioni 15 kwa kila kundi.
Miradi na
vigezo vya michanganuo hiyo vinalenga sekta ya elimu, afya na makundi
yaishio katika mazingira magumu, DSG inahamasisha dhana ya kuepuka
utegemezi, uwazi na uwajibikaji.
Baadhi ya miradi iliyofadhiliwa kwa mwaka uliopita ni pamoja na ujenzi wa uzio wa kituo cha watoto yatima cha Kidzcare (Bagamoyo), ukarabati wa samani kwenye Shule ya Sekondari ya wanawake ya Loreto (Mwanza), na utoaji wa vitabu na kamusi kwa wasichana wanaotoka jamii ya wafugaji wa kituo cha Emusoi (Arusha).
Wengine walionufaika na mradi huo ni kikundi cha Makini cha Dar es Salaam ambao husaidia watoto wa mitaani kwa kuwapatia mahitaji muhimu, mradi wa Neema Crafts Centre
kutoka Iringa unaosaidia watu wenye ulemavu kwa kuwapa mafunzo
yanayowawezesha kujiajiri pamoja na kikundi cha wananwake wa kazi za
mikono kutoka Kagera chenye lengo la kuwawezesha wanawake kujikomboa
kiuchumi.
Maonyesho
ya mwaka huu yanatarajiwa kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka vikundi
mbalimbali nchini, ambao watatoa maelezo na kuonyesha ubunifu wao kwa
jamii.
Mwenyekiti
wa kundi la wake wa Mabalozi (DSG), Julliana Parroni, ameeleza kuwa “
Michango yetu ni midogo ila inatumika kwa umakini mkubwa na kulenga
miradi ambayo inaonekana kukosa kipaumbele kwa wachangiaji wakubwa, ila
inaendeshwa vizuri na inanafasi ya kuleta maendeleo endelevu na
mabadiliko ndani ya jamii.”
Burudani
zitakazo kuwepo katika siku hiyo itatolewa na kundi la wasanii kutoka
Jamhuri ya Ireland na India, Kundi la sanaa la Makini na safi, Muziki wa
asili kutoka Tanzania na bendi ya Afrikwetu ikiwa ni mojawapo. Balozi
mbalimbali zitafanya maonyesho ya vyakula na zawadi kutoka sehemu
mbalimbali duniani.
No comments:
Post a Comment