ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, January 14, 2013

Safari ya miaka 18 bila kupumzika inaanzia hapa

Mwanangu Mary-Sia akiwana mama yake tayari kuanza siku yake ya kwanza shule ya chekechea akiwa a miaka miwili na miezi sita.

Mary-Sia akibembelezwa walao kunywa kikombe cha maziwa ambayo amezoea kunywa saa tatu lakini leo anakunywa saa moja ili kuwahi shuleni

Akiingia kwenye gari tayari kwa safari ya shule
  
Lango kuu la Shule St Josephine Bakita, wazazi mbalimbali wakiuku ya kuwapeleka watoto wao shule, wengine mara ya kwaangine wanaingia mwaka wa pili

Mama Sia akimkabidhi mwanaye kwa mlezi wa shule

Mary-Sia akiwa tayari na kundi la wenzake kuanza safari yake ya miaka 18 ya maisha ya masomo bila kupumzika


Watoto wakichangamshwa na walezi wao

Mary-Sia akichezwa na machale kuwa sasa anaachwa kwa mara ya kwanza mikononi mwa watu asiowajua

Mary-Sia akilia kutaka kuondoka na wazazi wake
  
Mtoto mwingine anarudishwa na mlezi baada ya kutoroka kutaka kuwafuata wazazi wake



Palikuwa hapatoshi kila mzazi/mlezi anahakikisha mwanae amekabidhiwa kwa walezi

Parking ilikuwa ni ya taabu ghafla.

Kama nilivyoweka katika kichwa cha habari, "Safari ya miaka 18 bila kupumzika inaanzia hapa"
Ni wakati ambapo Mama Sia na mimi tunaangalia nyuma tulikotoka. Tulipomwacha mtoto shuleni na kuelekea kazini, njiani tulikuwa tunajadili, hivi itachukua muda gani mpaka  Mary-Sia aweze kusimama na miguu yake mwenyewe kama Mungu atampa uzima? Hapo tulianza kuhesabu
1.Chekechea miaka miwili 2013-2014
2.Primary School 2015 - 2021
3. Form One - Form Four 2022-2025
4.Form Five-Six 2026-2027
5. JKT 2028?
6.Chuo Shahada ya kwanza 2029-2031

Hiyo ni miaka 18 bila kupumzika na kwa muda wote huo atakuwa anategemea wazazi asilimia 100%
Hivyo hata topic ya uzazi wa mpango ikaingia. Hivi kwa ughali wa elimu ya sasa hivi itatugharimu kiasi gani kwa miaka hiyo 18?  Bila shaka inategemea na aina ya shule unayompeleka mwanao lakini kama ni shule hizi ambazo walao zinaitwa shule basi ujue gharama ya chekechea, primary na sekondary hazitofautiani saana. 
Takriban kwa mwaka ni milioni 2 kama gharama za maisha hazitapanda miaka ijayo.
Hivyo ili mtu awe na uhakika wa kusoma miaka hiyo 18 inabidi baba na mama wafanye kazi ya ziada.
Wakati tulipomzaa Mary-Sia tulimfungulia Junior account ambamo tumekuwa tunamwekea akiba. Tumegundua kuwa akiba hiyo haiwezi kuzaa riba ya kutosha kumwendeleza kimasomo mpaka atakapotimiza miaka 18 ya shule. Hicho tumejadili namna ya kubuni mradi ambao utaweza kutunisha mfuko wa Mary-Sia ili kuwa na uhakika zaidi wa kukamilisha safari hiyo ya miaka 18 bila kupumzika. 
Tufungue duka la rejareja? au la jumla? Tufuge kuku? tukalime? Maana kwa hakika mshahara hautoshi na bado tunahitaji kuongeza mtoto mwingine walao mmoja. Tutafanyaje? Hii ndiyo hali halisi ya maisha ya asilimia kubwa ya Watanzania wengi. Tumepeana homework na mama sia ili hadi Jumamosi tuwe na jibu la nini cha kufanya ili mtoto wetu aweze kudumu katika safari yake ya miaka 18 bila bughudha ya aina yeyote.
Tutakapopata ufumbuzi wa hilo tutakujulisha

Na Mdau Bahati

(Video yake)

 




No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...