MTOTO WA MIAKA 4 DEVOTHA GERLAD ALIYEKATWA MAPANGA NA BABA YAKE,HAPA AKIWA HOSPITALI KWA HUDUMA AYA
KWANZA.
ASKARI POLISI
MSTAAFU SAMSON BWIRE AKIWA AMEFIKISHWA HOSPITALINI MDA MCHACHE BAADA YA KURUKA
KUTOKA KWENYE GARI AKIJARIBU KUKIMBIA.
MTOTO WA MIAKA 4
DEVOTHA GERLAD ALIYEKATWA MAPANGA NA BABA YAKE,HAPA AKIWA HOSPITALI KWA HUDUMA
AYA KWANZA.
WANANCHI WAKIWA NJE
YA HOSPITALI YA WILAYA WAKIWA NA SHAUKU YA KUMUONA MTUHUMIWA.
KINA MAMA
WALIOGUSWA NA TUKIO WAKIWA NJE YA HOSPITALI KUMUONA MTOTO HUYO.
AFANDE BWIRE AKIWA
HOI WODINI
HAPA AFANDE AKIWA
HOI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALINI..
MADAKTARI
WAKIJITAHIDI KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.
MADAKTARI WAKIWA
KAZINI KUHAKIKISHA WANAOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.
JITIHADA ZA KUOKOA
MAISHA YA MTOTO ZIKIENDELEA
INASIKITISHA SANA
JAMANI
MAJUKUMU YA KUOKOA
MAISHA YA MTOTO HUYO YAKISONGA KWA KASI.
AFANDE BWIRE AKIWA
NA PINGU ZAKE WODINI
MUNGU AMPE AHUENI
MTOTO HUYU.
WANANCHI WAKIWA NJE YA HOSPITALI YA WILAYA WAKIWA NA SHAUKU YA KUMUONA MTUHUMIWA.
AFANDE BWIRE AKIWA HOI WODINI
KAHAMA.
Mkazi wa kitongoji cha Sango kata ya
Nyasubi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga Samson Bwire (54),
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumcharanga mapanga mtoto wake
Devotha Gerald (4) kwa sababu za wivu wa kimapenzi.
Tukio hilo limetokea leo jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana na mke wake Happiness Elius (28) huku
akiwa amelewa pombe ambapo, mkewe alikimbia kitu kilichosababisha
kumgeukia mtoto Devotha na kuanza kumkata mapanga kichwani.
Kwa mujibu wa majirani, kelele
zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba walipoenda walimkuta Bwire
akichoma nguo za mke wake, na alipowaona aliingia ndani na kuanza
kumkata mapanga mtoto huyo huku akiwa amefunga mlango.
Imefafanuliwa kuwa, baada ya kusikia
kelele za mtoto, majirani walianza kuvunja milango huku wakiomba msaada
kituo cha Polisi na baada ya Polisi kufika walifanikiwa kumnusuru
mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani.
Majirani kwa hasira walianza kumpiga
Bwire ambaye ni askari polisi mstaafu wa cheo cha koplo kwa nia ya
kumwua, hali ambayo imelipa jeshi la Polisi kazi ya ziada kumnusuru na
kumpakia kwenye gari kwenda kituoni.
Hata hivyo Wakati gari la Poisi likiwa
katika mwendo wa kasi eneo la soko la Mkulima, Bwire ameruka kutoka
kwenye gari na kuangukia kwenye Lami kitendo kilichomsababishia
majeraha makubwa sehemu za usoni.
Mtoto Devotha na baba yake Bwire wote
wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu huku Bwire
akiwa Chini ya Ulinzi mkali wa polisi.
No comments:
Post a Comment