Mwandishiwa makala hii alikuwa ni mmoja wa waamini waliotembea na
kutembelewa na msalaba huu. Kilichonigusa kuandika makala hii ni jinsi
ambavyo watu baki, yaani majirani wa madhehebu mengine walivyokuwa nao
kwa namna moja ama nyingine walikuwa wakifurahia na kutabasamu na
kupunga mikono kila tulipopita na msalaba wetu. Nikajiuliza moyoni; "Huu
mpasuko wa kidini tunaousikia siku hizi mara kwa mara ni nadharia au uko katika levo
nyingine"? Kiukweli Watanzania, hususan majirani zangu tunaoishi mtaa
mmoja, tunaofanya kazi pamoja, hakuna hata chembe moja ya udini.
"HAKUNA" Hata msikiti wa hapa kwetu pamoja na kuwa ni nyumba ya ibada lakini mbambo ya kijamii yakitokea kwa mfano mtoto amepotea au mtu amefiwa, shehe anawatangazia watu wote kuhusu tukio hilo bila kujali ni dhehebu gani. Mimi nilipohamia hapa kabla hata sijajua mazingira nilifiwa na mdogo wangu, shehe alikuwa kati ya watu wa kwanza kuja kutoa pole na muda ule ule alienda msikitini na kutoa tangazo na wajirani wakaitikia haraka sana, hadi leo inafanyika hivi. Hakuna Udini Tanzania, na wala sidhani kama utakuwepo siku za hivi karibuni, labda kwa vizazi vijavyo. Udini tunaousikia hasa haupo kwenye grassroots, kwa maana katika maisha ya kila siku ya mtanzania, walao mimi sikutani na vikwazo hivi, ukizingatia shughuli zangu zinanifanya nikutane na watu wa madhehebu mbalimbali kila siku. Sijawahi kukwazika au kukosa huduma muhimu kwa sababu ni Mkristo. Sijawahi kuhisi kukosa amani au uhuru wa kuabudu kwa sababu tu ni Mkristo, walau katika levo yangu, levo ya kawaida, na majirani zangu, na wanamtaa wangu. Tunaposikia siku hizi kwamba kuna mpasuko au kuna clashes za kidini, zinatoka wapi? Ni nani anazileta na kwa manufaa gani? Wananchi wa kawaida tuendelee kuishi katika misingi yetu ya ujirani na utaifa. Tusikubali kubeba bendera za udini ambazo malengo yake hatuyajui. Vijana tusikubali kurubuniwa kwa vijisenti vichache kwa nia ya kuharibu amani yetu. Wazee wetu na wazee wa wazee wetu waliishi hivi, "KWA AMANI"na sisi katika kizazi chetu tuitunze tunu hii ili tuwaachie watoto wetu na watoto wa watoto wetu tunu hii. Duniani tunapita na wengine wanakuja. Hata tukiwa na agenda gani tutapita tu. Mungu ibariki Tanzania na Watu wake.
Paroko wa Parokia ya Damu Takatifu Fr. Msuya akiadhimisha misa katika Jumuiya kuashiria kuanza kwa mkesha.
Mama akitoa mahubiri katika misa hiyo akishuhudia jinsi msalaba ulivyokuwa wokovu kwake na kwa familia yake
Wanajumuiya wakiwakabidhi Jumuiya nyingine msalaba baada ya kukesha nao
Wakristo wakatoliki wakiona fahari ya msalaba unapopita katika familia na mitaa yao
Wakristo wakatoliki wakifurahi baada ya kupata baraka.
Katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Msalaba unachukua maana ya pekee katika maisha ya waamini, kwani wanatumwa na kuchangamotishwa kuwa ni mashahidi amini wa Kristo na Kanisa lake: kwa maneno na matendo. Msalaba ni kielelezo cha mapendo, neema, sala, msamaha na matumaini yasiyodanganya kamwe!
Ndiyo maana, Kanisa linaona fahari juu ya Msalaba wa Kristo kwa kuutembeza katika nyumba za waamini, ili wapate nafasi ya kusali na kulitafakari Fumbo la Msalaba, ishala ya mateso na alama ya wokovu wa binadamu; mahali ambapo hekima ya Mungu imetundikwa juu yake! Ni mwaliko wa kutubu na kumwongokea Mwenyezi Mungu.
Hiyo ni alama ya kweli na wazi kuwa Watanzania wanasababishiwa matatizo na viongozi wao wenyewe ambao ndio vinara wa kueneza uchochezi wa kidini na hali wananchi wa kawaida wanaishi kama ndugu...big up mwandishi!
ReplyDelete