ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, July 25, 2013

Mambo ya Kichina: Mtoto wa mwaka mmoja abeba ujauzito.

1-Year-Old Chinese Girl Pregnant With Her Twin In Her Womb

Wazazi wa Kang hawakuelewa mara moja ni kwa nini tumbo la mtoto wao wa mwaka mmoja alikuwa na kitambi ambacho si cha kawaida na kilikuwa kinakuwa kila siku.

Tumbo la Kang lilionekana na dalili zote za ujauzito kitu ambacho kilifany amajirani waanze kujiuliza kulokoni hadi kumpa jina la "Monster"

Lakini baada ya madaktari kumfanyia uchunguzi mtoto huyo ambaye ana miezi 18 tu waligundua kuwa alikuwa na hali ambayo si ya kawaida kabisa ambayo inatokea mara moja kati kesi  500,000 za kujifungua. Hii inatokea wakati mama mjamzito akiwa amemeba mimba ya mapacha, pacha mmoja kukuwa kiukubwa kuliko pacha mwenzake na kummeza pacha mdogo. Kwa maana hiyo kitoto kingine (foetus) hakikui ila kinakulia ndani ya tumbo la pacha mkubwa kama parasite.

Hali hii ilimfanya Kang anayetokea katika jimbo la Henan, ashindwe kula vyakula vigumu na apatwe na maumivu makali wakati wote.

Hata hivyo, Kang anaelezwa kuwa ni mtoto wa majanga kwani akiwa na siku chache tu tangu kuzaliwa, wazazi wake walimwacha shambani, kilio chake ndicho kilichopelekea mfanya kazi wa shambani Wang Ghihua kumchukua na kuishi naye kwani yeye na mume wake Kang Xiqung hawakuwa na mtoto hivyo wazai wa Kang wakawaruhusu kukaa naye. Walezi walishituka kuambiwa kuwa Kang alikuwa na kitotot tumboni ambacho kilikuwa kikikandamiza viungo vyake vya ndani kadiri mimba ile ilivyokuwa inakuwa.Kang alihitaji upasuaji ambao ungegharimu paundi 1,000 tu lakini walezi wake walikosa, hadi msaada kutoka Msalaba Mwekundu ulivyowasili na kuchangisha pesa kwa ajli ya kumfanyia Kang upasuaji. Upasuaji ulichukua saa 10 na katoto kale kengine kalitolewa tumboni na sasa Kang anaendelea kupata nafuu ya ile opereshen na atarudi kwenye maisha yake ya kawaida. Hata hivyo upasuaji huu haukuathiri mfumo wake wa uzazi hivyo akifikia utu uzima ataweza tena kupata watoto kama kawaida.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...