ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, July 22, 2013

MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSUTOZO YA KODI YA LINE ZA SIMU

 





SERIKALI imesema msimamo wa serikali kuanzisha tozo ya kodi katika laini za simu hautabadilika kutokana na ulazima wa kupata fedha kwa ajili ya kuunganisha umeme maeneo ya vijijini ambako bado watu wengi wanaishi bila umeme.

Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda alipokuwa akihutubia wananchi na viongozi mbalimbali kwenye mkutano uliofanyika katika viunga vya Halmashauri ya Manispaa ya Songea.


Mizengo Pinda alisema kuwa kodi ya laini imewekwa mahususi ili kukusanya fedha ambazo zitatumika katika kuunganisha umeme kwenye maeneo mengi hususani ya vijijini ambayo kwa sasa hayana umeme jambo ambalo alisema linakwamisha jitihada za wananchi kujiletea maendeleo ambapo alisema kila mtumia laini ya simu atapaswa kulipa kodi ya shilingi elfu moja kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...