ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, July 18, 2013

Rais Kikwete anastahili pongezi - Lowassa


Mheshimiwa Edward Lowassa
Photo swahili TV



Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Edward Lowassa, amemsifia Rais Jakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata heshima katika ulingo wa kimataifa, aliyasema hayo wakati akihojiwa na Swahili TV jijini Washington DC.


Alisema kitendo cha Rais wa Marekani Bwana Barack Obama kuja nchini na viongozi mbalimbali wa mataifa makubwa kumeonyesha Rais Kikwete anakubalika.


“Ni hivi karibuni tu Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani George W. Bush walikuwa nchini Tanzania, hii inaonyesha kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa” alisema Mheshimiwa Lowassa.


Mheshimiwa Lowassa ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi, aliongeza kwa kusema, Rais Kikwete anastahili pongezi sana kwa hilo kwani sio rahisi kwa viongozi wa mataifa makubwa kutembelea nchi zingine labda kama mko juu sana katika medani za kimataifa.



Pia alisema Rais Kikwete amekuwa akihusishwa na utatuzi au ushauri wa kutatua matatizo mbalimbali ya nchi zingine na pia ameanza kuishirikisha Tanzania katika usimamizi wa amani katika nchi mbalimbali.


Tanzania iliweka historia hivi karibuni kwa maraisi wawili wa Marekani kukutana katika nchi moja kwa wakati mmoja, Rais Barack Obama na George W.Bush walikutana jijini Dar es Salaam mwezi huu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...