Katika swali
hilo, Magige aliitaka Serikali ieleze ukubwa wa biashara ya dawa za kulevya
nchini na ukoje na kuhoji kama haioni kuna tatizo katika ukaguzi wa abiria na
mizigo kwenye viwanja vya ndege wanakopita watuhumiwa.
Mbunge huyo pia
aliitaka Serikali, ieleze imefanya juhudi gani za kukabiliana na hali ya
upitishwaji wa dawa hizo.
Akijibu swali
hilo, Lukuvi alisema ukubwa wa biashara hiyo nchini, unadhihirishwa na idadi
hiyo ya watuhumiwa Watanzania wanaoshikiliwa nje ya nchi kuanzia 2008 hadi Julai
2013.
Mbali na
Watanzania hao nje ya nchi, Lukuvi alisema nchini kuna wageni wapatao 31
wanaoshikiliwa mahabusu katika magereza ya Keko na Ukonga.
Baada ya kutoa
ufafanuzi huo, Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse (Chadema), aliomba
kuuliza swali la nyongeza ambapo aliitaka Serikali kutaja kwa majina wahusika
katika biashara ya dawa za kulevya.
Akijibu swali
hilo, Lukuvi alisema kazi ya Serikali si kutaja majina, bali kuyapokea na
kuyafanyia uchunguzi na mwisho kuchukua hatua za kisheria.
“Si kazi ya
Serikali kutaja wahusika bungeni, lakini tunachofanya kwa ambao wanatajwa ni
kuwapeleka katika vyombo husika na kuendelea na uchunguzi na wakithibitika ndipo
wanatajwa na kuchukuliwa hatua.
“Tukisema
tuwataje, hata humu ndani wabunge wote watakwisha maana wako kwengi
wanaotajatajwa. Hata gazeti la Jamhuri limetaja maana wenzetu wanao ushahidi
nao, na wale wasioridhika wanaweza kwenda kushitaki.
Hivyo walio na
majina na vielelezo watuletee ili tuwashughulikie. Baadhi ya wabunge walionekana
kuguna na kuzomea pale Lukuvi alipokuwa akitoa ufafanuzi wa suala hilo, jambo
lililomfanya Spika Anne Makinda, kukemea hali ya zomeazomea ndani ya
Bunge.
Hivi karibuni,
vita dhidi ya dawa za kulevya, imekuwa gumzo baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk
Harrison Mwakyembe kuapa kuzuia uchochoro wa kupitisha dawa hizo katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Kwa kuanzia, Dk
Mwakyembe alitaja maofisa alioagiza wafukuzwe kazi na kufunguliwa mashitaka ya
jinai chini ya Sheria ya Kuzuia Dawa za Kulevya, kwa tuhuma za kupitisha dawa za
kulevya katika uwanja huo.
Maofisa hao ni
pamoja na Maofisa Usalama, Yusufu Daniel Issa, Jackson Manyonyi, Juliana Thadei
na Mohamed Kalungwana. Mbali na maofisa hao, pia aliagiza Jeshi la Polisi
kumwondoa mara moja katika uwanja huo, askari Polisi, Koplo Ernest na
kumchukulia hatua za kinidhamu kwa kushiriki kwake kwenye njama za kupitisha
mabegi sita ya dawa za kulevya, yaliyokamatwa Afrika Kusini.
Pia alisema
Polisi inapaswa kumsaka Nassoro Mangunga, aliyekwepa vyombo vya Dola vya Afrika
Kusini na kutoroka na mabegi matatu ya dawa hizo. Dk Mwakyembe alisema mbeba
mizigo katika uwanja huo, Zahoro Seleman, anapaswa kufukuzwa kazi, kukamatwa na
kufunguliwa mashitaka, ili aunganishwe na wenzake kujibu mashitaka ya
jinai.
Dk Mwakyembe pia
aliiagiza Idara ya Usalama wa Taifa kuendesha uchunguzi wa kina kwa maofisa wake
waliokuwa zamu siku ya tukio, kwa kuchelewa kufikisha mbwa wakati mwafaka
kukagua mabegi hayo na kuliletea Taifa fedheha kubwa.
No comments:
Post a Comment