Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema nchi yake haitishwi na hatua iliyochukuliwa na serikali ya Marekani, kusitisha msaada wake wa kijeshi kwa nchi hiyo, kwa kile inachodai Rwanda inawafadhili waasi wa M23 wanaopigana na serikali mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.
Rais Kagame amesema anashangazwa na hatua ya Marekani kuihukumu
nchi hiyo kwa makosa ambayo Rwanda haihusiki kwa lolote wala haifadhili
kundi lolote la waasi nchini DRC na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni
kutoitendea haki Rwanda. Rais Kagame amesema kamwe Rwanda
haijawahi kuhusisha watoto wadogo kwenye jeshi lake wala kuunga mkono
kutumikishwa kwa watoto wadogo kama wanajeshi kwenye kundi la M23. Serikali
ya Marekani ilitangaza majuma kadhaa yaliopita kusitisha msaada wake wa
kijeshi kwa serikali ya Rais Kagame kufuatia hatuwa hiyo inayotajwa ya
kuwafadhili waasi wa kundi la M23 wanaopambana na serikali ya Rais
Joseph Kabila.

No comments:
Post a Comment