
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watatu kushoto) na
baadhi ya viongozi katika msafara wake, wakishiriki Nov 20, 2013, kungoa
magugu na visiki, kuandaa shamba la mfano la wanawake na vijana
wajasiriamali katika kijiji cha cha Mkwaya Kata ya Kilimani wilayani
Mbinga mkoani Ruvuma, alipotembelea shamba hilo lenye ukumbwa wa ekari
500. Mbali na kushiriki kazi hiyo Kinana alitoa mchango wa sh. 400,000
kwa ajili ya mafuta ya trekta ya kulimia shamba hilo. Baadhi ya viongozi
wengine ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose
Migiro (kulia).

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akikagua
mradi wa mgodi wa makaa ya mawe wa kampuni ya Tancoal katika eneo la
Mtunduwalo, Mbinga mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013. Kinana alitembelea mgodi
huo, kufuatia mgogoro uliopo kati ya wananchi na uongozi wa mgodi
kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo malipo ya fidia kwa maeneo
yalitochukuliwa.

Kijana Bonus Hyera wa kijiji cha Lusewa,
akimsalimia kwa kumbusu
mikono kwa shauku, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk.
Asha-Rose Migiro, baada ya Dk. Asha-Rose kukutana na kijana huyo, wakati
wa shughuli ya uzinduzi wa tawi la CCM Kata ya Mbinga mjini, mkoani
Ruvuma, Nov 20, 2013, uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana. Kijana huyo aliyeonekana kama aliyekuwa amelewa kiasi,
alionyesha heshima kubwa kwa Dk. Asha-Rose, tofauti ilivyokuwa
inadhaniwa na baadhi ya watu waliopomuona akimsogelea kwa shauku
kiongozi huyo.

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose
Migiro (kushoto) akimpongeza Balozi wa shina, Hilda Komba, baada ya
kikao cha wanachama kilichofanyika kwenye balozi huyo, Nov. 20, 2013,
Kata ya Amani Makolo, Mbinga mkoani Ruvuma.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
akiijaribu pikipiki wakati akikabidhi pikipiki katika awamu ya pili ya
mradi wa pikipiki 50 za vijana waendesha bodaboda kwa mwenyekiti wa
kundi la waendesha bodaboda hao,
Alkhass Ramadhani(katikati), wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika,
mjini Mbinga, Nov 20, 2013. Pikipiki hizo zimetolewa na Mbunge wa Mbiga
Mashariki, Ndugu Kayombo. Kulia ni Katibu wa NEC, Itrikadi na Uenezi,
Nape Nnauye.

Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana (wapili kushoto), baada ya Kinana kuwakabidhi kadi
katika kikao kilichofanyika nyumbani kwa balozi Hilda, Kaya ya Amani
Makolo, Mbinga mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013. Zaidi ya wanachama 50 walipokea kadi hizo.

Katibu Mkuu wa CCM na msafara wake, wakitazama ngoma ya mganda,
kabla ya mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa michezo mjini
Mbinga mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013.

Wananchi wakiselebuka, wakati wa shamrashamra za kumlaki Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili kwenye Uwanja wa Michezo
mjini Mbinga, Novemba 20, 2013.

Balozi wa shina namba 29, Kata ya Amani Makolo, Mbinga,mkoani
Ruvuma, Hilda Komba akifungua kikao cha wanachama, ambacho Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) alihudhuria, Nov 20, 2013. Katibu wa
NEC,ltikadi na uenezi, Nape Nnauye (watatu kulia- waliokaa), alihudhuria
kikao hicho.

Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye akiliraibu kwa
kulipiga buti, tairi la gari yake kujua kama lilikuwa limetengemaa,
baada ya kupachikwa na dereva wake (hayupo pichani) gari hilo lilipokuwa
limepata pancha katika kijiji cha Lusewa, Kata ya Mbinga Mjini, wakati
msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliokuwa katika kata
hiyo, Nov 20, 2013.Picha Zote na Bashir Nkromo
No comments:
Post a Comment