MATA AKABIDHIWA JEZI NAMBA 8 MAN UNITED
KIUNGO Juan Mata ametambulishwa Manchester United na kukabidhiwa jezi namba nane (8).
Ilitarajiwa
Mspanyola huyo angepewa jezi maarufu Old Trafford, namba saba (7),
afuate nyayo za Cristiano Ronaldo, David Beckham, George Best na Eric
Cantona. (HM)
Lakini mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa
Pauni Milioni 37, kiwango kikubwa zaidi United kutoa kununua mchezaji
kihistoria, amechukua namba nane 8, ambayo mara ya mwisho alivaa
Anderson, aliyehamia Fiorentina kwa mkopo.
Tetesi kwenye Twitter zinasema jezi
namba saba (7) amewekewa Cristiano Ronaldo atakaporejea mwishoni mwa
msimu. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment