Mke wa aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Said Bwanamdogo, Pili Mohamed
(katikati) akiwa nyumbani kwake eneo la Makondeko Mbezi Dar es Salaam,
jana. Picha na Michael Jamson.
*******
Mbunge wa Chalinze, Said Bwanamdogo anazikwa leo kijijini
kwake, Miono Bagamoyo, maziko yanayotarajiwa kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa chama na Serikali.
Kifo cha mbunge huyo ni pigo la pili ndani ya
mwezi mmoja baada ya kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Kalenga, mkoani
Iringa, Dk William Mgimwa.
No comments:
Post a Comment