Rais wa Marekani Barack Obama
atakutana na Papa Francis huko Vatikan wakati wa ziara yake ya wiki moja
Ulaya iliyopangwa kufanyika mwishoni mwa Machi.
White House inasema rais Obama
anatarajia kuzungumza na Papa Francis kuhusu mtizamo wao unaolingana
katika kupambana na umasikini na tofauti ya kipato inayoendelea
kuongezeka.
Mkutano huo umepangwa kufanyika Machi
27 .Wakati akiwa Roma rais Obama anapanga kukutana na rais wa Italia
Giorgio Napolitano na waziri mkuu Enrico Letta.
Kiongozi huyo wa Marekani ataanza
ziara yake ya Ulaya huko The Hague Uholanzi ambako atashiriki katika
mkutano wa usalama wa nyuklia ulioandaliwa na serikali ya Uholanzi.
Chanzo, voaswahili.com
No comments:
Post a Comment