Mwakilishi kutoka Ubalozi
wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa
mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongelo ya Singida, Jafari Ndagula
mmoja wa washindi wawili wa jumla wa shindano la Wanasansi Chipukizi
Tanzania 2013 (YST) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Jafari na mwenzake Fidel Samwel (hayupo pichani) wataiwakilisha Tanzania
katika sherehe za Tuzo za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani
mjini Dublin Ireland. Tuzo za YST zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland
kwa kushirikiana na Mfuko wa Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine
kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na
Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF, Hatim Karimjee.
.Shirika la Irish Aid na Taasisi Karimjee wadhamini safari na udhamini wa masomo chuo kikuu
Na Damas Makangale, MOblog
SHIRIKA
la Irish Aid kwa kushirikiana na Taasisi ya Karimjee Jivanjee “KJF” kwa
kufadhili wanafunzi wanne bora toka shule ya sekondari ya Ilongero ya
Singida na Fidel Castro ya Pemba kwenda Dublin, Ireland baada ya kuibuka
washindi wa jumla katika mashindano ya wanasayansi chipukizi (Young
Scientists Tanzania) YST mwaka 2013.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa udhamini na kuwaaga rasmi wanafunzi
wao jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Taasisi ya karimjee
Jivanjee, Hatim Karimjee amesema kwamba wanafunzi wawili kutoka shule
ya sekondari ya Ilongelo, Jafari Ndagula na Fidel Samwel walishinda tuzo
za jumla katika mashindano ya YST 2013 kwa kufanya utafiti wa mradi wa
kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya kutumia matone (Recycled Material)
“washindi
walipokea zawadi ya fedha taslimu, medali, laptops na sasa ziara ya
kwenda Dublin Ireland kuwawakilisha wanafunzi wa kitanzania katika
sherehe za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani,” amesema karimjee
“Washindi
pia walipata udhamini kutoka Karimjee Jivanjee Foundation kwa ajili ya
masomo yao ya chuo kikuu kwa siku zijazo kama sehemu ya jitihada za
msingi za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi ya
Tanzania,” alilisitiza.
Amesema
kuwa YST pia iliwapa tuzo wanafunzi wawili , Muslih Othman Khamis na
Amne Said Sauti kutoka shule ya Sekondari ya Fidel Castro kutoka Pemba
kwa ajili ya utafiti wao wa kisayansi juu ya (ethanol) kwa kutumia miwa.
“matokeo
ya utafiti wao yatasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira kwa watu
badala ya kutumia kuni au mkaa au kutumia pesa nyingi kununua mafuta ya
taa, wanaweza kutumia ethanol iliyotengezwa kutokana na miwa ambayo
inapatikana kwa wingi huko Pemba,” amesema
”
KJF wamekuwa wakisaidia YST tangu 2012 na kuwa mdhamini mkuu na mwaka
2013 KJF waliongeza msaada wake kwa YST kwa kutoa udhamini kwa washindi
wa ujumla ikiwa ni pamoja na masomo ya juu kwa ajili ya wale
wanaohitaji,” aliongeza.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Ofisi ya Kamishina wa Elimu, Hadija Mcheka amesema kuwa serikali
inaunga mkono kwa ukamilifu mpango ulioanzishwa na YST kwa sababu
itaweza kukuza na kuhamasisha wanafunzi kujiingiza katika masomo ya
sayansi.
”Programu
Hii itakuwa inakuza na kuhamasisha ubunifu miongoni mwa wanafunzi
katika nchi wakati jukwaa hili pia litasafisha njia kwa ajili ya
wanafunzi kuja pamoja na na kubadilishana uzoefu, ” alieleza.
YST
Mkurugenzi Dk Gosbert Kamugisha amesema kuwa waliamua kuja na mpango huo
kutokana na ukweli kwamba matokeo ya kidato cha nne na sita kwenye
masomo ya sayansi yalikuwa yakishuka siku hadi siku.
Amesema,
” YST ” iliwakutanisha wanafunzi 120 na 60 kutoka shule za sekondari
katika mikoa ipatayo 18 na mashindano hayo yalifanyika mwezi wa Septemba
mwaka jana.
Dkt
Kamugisha amesema mpango huo ni jukwaa murua kwa wanafunzi wa shule za
sekondari kuja pamoja kuchunguza nadharia, kugundua teknolojia mpya na
kuendeleza elimu kisayansi kwa njia ya utafiti na uvumbuzi.
“Kwa
vitendo mpango wa kulea wanasayansi vijana kutoka hatua mapema na
kuelimisha umma kwa ujumla juu ya umuhimu wa sayansi katika maisha ya
kila siku na maendeleo ya kiuchumi, ” amesema.
No comments:
Post a Comment