Anatory
Amani amenukuliwa akisema katika mahojiano na STAR TV usiku wa Januari
22, 2014 kuwa hajawahi kutamka kujiuzulu na sio kweli kuwa amejiuzulu.
Akaongeza kuwa hawezi kujiuzulu kwakuwa hajafanya kosa lolote na CAG
alitoa hati safi kwa manispaa yake 2012/13, hivyo, ni kwa nini leo aseme
yeye ni fisadi? Anasema yeye anaendelea kufanya kazi zake kama kawaida
akiwa Meya halali wa manispaa ya Bukoba: “Mimi sijajiuzulu. Siku ile
baada ya ripoti ya CAG kusomwa mimi niliambiwa niseme neno na Naibu
Waziri, nikasimama nikainua mikono juu na kusali Zaburi 23 ninayoifahamu
kwa kichwa.”
Ifuatayo ni sehemu ya taarifa inayolandana na kufafanua nukuu hiyo, kama ilivyochapishwa katika moja ya magazeti ya leo:
LICHA
ya kutangaza kujiuzulu kwa agizo la serikali baada ya ripoti ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Uttouh,
kumtia hatiani aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani,
ameng’ang’ania kiti hicho.
Januari 17, mwaka huu, Amani alikubali agizo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya CAG kuthibitisha kuwa

miradi aliyokuwa akiitekeleza katika manispaa hiyo ilikiuka utaratibu na haikuwashirikisha madiwani.
Mbali na Amani, wengine waliowajibishwa kwa kuvuliwa madaraka ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Hamis Kaputa, aliyekuwa amehamia Mbeya, Mhandisi wa Halmashauri, Steven Nzihirwa na Mhasibu, Hamdun Ulomy.
Katika hali ya kushangaza, juzi Amani aliandika barua kwenda kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo, akimwarifu kuwa hatakuwepo kwa wiki sita, hivyo majukumu yake yatatekelezwa na naibu meya.
Nakala ya barua hiyo ya Januari 12, 2014 yenye kumb. Na. BMC/R.30/MEYA/Vol.II/526, ilitumwa pia kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Katibu Tawala wa Mkoa, Mkuu wa Mkoa, Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera na Naibu Meya, Alexander Ngalinda.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka mjini Bukoba jana zilisema kuwa barua hiyo yenye kichwa cha habari: ‘Yah: Kusafiri kumpeleka mtoto wangu kwenda kutibiwa,’ ilizua taharuki kwa baadhi ya wakazi wa Bukoba, wakihoji kama Amani amerukwa akili au la.
Barua hiyo ilisomeka: “Nakujulisha kuwa sitakuwepo kwa takriban muda wa wiki sita. Nampeleka mtoto wangu kwenye matibabu ya moyo (Congenital Cardiac Mulfunction). Kwa muda ambao sitakuwepo, Naibu Meya afanye majukumu yote ya Meya. Ikiwa ni pamoja na kuendesha vikao hadi nitakaporudi,” alisaini Dk. Anatory Amani akijitambulisha kama Meya wa Manispaa ya Bukoba.
Gazeti hili lilimtafuta Amani ili kupata ufafanuzi juu ya barua hiyo lakini simu yake iliita bila kupokewa, hata ujumbe mfupi alioandikiwa hakuujibu.
Mkuu wa Mkoa, Fabian Massawe, alisema serikali na jamii kwa ujumla inatambua kuwa Amani alijiuzulu kama meya Januari 17, baada ya taarifa ya CAG.
“Kwamba barua aliyomwandikia mkurugenzi imefanyiwa kazi na ngazi ya serikali ya mkoa na wilaya. Malumbano ya kisiasa yamewachosha wananchi na kurudisha maendeleo nyuma, kwa sasa basi,” alisema Massawe.
Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya, Zipora Pangani, alisema hata yeye nakala ya barua hiyo aliipata jana, hivyo alikuwa bado anafuatilia na kuomba kwa sasa aulizwe Mkurugenzi, Shimwela L.E, ambaye hakupokea simu wala kujibu ujumbe mfupi.
---
Hii ni sehemu ya taarifa iliyonukuliwa kutoka kwenye gazeti la TanzaniaDaima

No comments:
Post a Comment