JANA February 25 Uongozi wa hospitali ya taifa muhimbili kwa kushirikiana na
maafisa wake wa usalama wamemnasa daktari feki aliyekuwa akiwatapeli
fedha wagonjwa na watu mbalimbali wanaofika kwa ajili ya kupatiwa huduma
za matibabu katika hospitali hiyo.
Taarifa
kutoka Muhimbili inasema ni Tukio la tatu kutokea katika hospitali hiyo
ingawa matukio ya namna hiyo yameshawahi kuripotiwa katika baadhi ya
hospitali kubwa za serikali kwa baadhi ya watu wanaotumia mwavuli wa
fani ya udaktari kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Msemaji wa Hospital ya taifa
Muhimbili Aminieli Aligaesha amemtaja Daktari huyo feki kwa jina la
Kitano Mustapha na kubainisha kuwa katika upekuzi uliofanywa na maofisa
usalama wa hospitali hiyo wamemkuta mtuhumiwa akiwa na kadi tatu za
kliniki,namba za simu za madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo huku
wakitambua kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria zilizopo na
kanuni za utabibu.
Daktari huyo feki Kitano
Mustapha amekana kutohusika na utaperi huo kwa wagonjwa mbali mbali
wanaofika kupata huduma za kimatibabu na kusema hawezi kuongea lolote
mpaka Mwanasheria wake awepo
No comments:
Post a Comment