ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, February 12, 2014

IGP Mstaafu Said Alli Mwema Kuagwakwa hafla maalum Jumamosi Tarehe 15 February 2014 katika viwanja vya Polisi Barracks Barabara ya Kilwa


 IGP Mstaafu Said Alli Mwema 
--
Jeshi la Polisi nchini, linapenda kuufahamisha umma kuwa, mnamo tarehe 15/02/2014 siku ya Jumamosi katika viwanja vya Polisi Barracks, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, kutakuwa na hafla ya kumuaga IGP Mstaafu Said Alli Mwema kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana.

Katika hafla hiyo, kutakuwa na mambombalimbali yaliyoandaliwa ikiwemo gwaride   maalum la heshima.

Ikumbukwe kuwa, katika kipidi chake cha uongozi wa Jeshi la Polisi, IGP Mstaafu Said Alli Mwema alishirikiana vyema na wananchi wa kada zote wakiwemo wadau mbalimbali wa amani, hususani katika dhana ya Ulinzi shirikishi na Polisi Jamii. Jeshi la Polisi nchini kwa kulitambua hilo, linatumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wote kuhudhulia hafla hiyo. 

Aidha, IGP Mstaafu Said Alli Mwema katika uongozi wake alianzisha na kusimamia mifumo mbalimbali ya kuzuia na kukabiliana na uhalifu hapa nchini ikiwemo maboresho ndani ya Jeshi la Polisi, ili kuhakikisha Jeshi linafanya kazi kwa weledi, usasa na ushirikiano na wananchi. 


Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...