
February 2014
MAHAKAMA KUU YAHAIRISHA KESI YA LULU
KATIKATI LULU AKIWA MAHAKAMANI KUSHOTO NI MAMA YAKE MZAZI KULIA NI DR CHENI
Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili msanii wa kike wa filamu Tanzania Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu
akituhumiwa kumua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba imetajwa leo
mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam.Mnamo tarehe 7/4/2012 huko sinza
vatican Dar es Salaam mtuhumiwa bila makusudi alimua Steven
Kanumba.Mshitakiwa na marehemu walikua na uhusiano wa penzi.Siku ya
tukio mshtakiwa alienda kumtembelea marehemu nyumbani kwake sinza
akawakuta marehemu na mdogo wake Setty Bosco wakijiandaa kutoka saa
12.00pm ya usiku.Ndipo mshtakiwa alifika nakuingia ndani kwenye chumba
cha marehemu.Mdogo wa marehemu akasikia malumbano kati ya Lulu na
Kanumba kwa nini anapokea simu za watu wengine.Baada ya hapo lulu
akataka kutoka nje marehemu akamvuta arudi ndani .Baada ya hapo lulu
akatoka nje akiwa analia na kumuambia Setty Kanumba ameanguka
chini.Ndipo Setty Bosco akawasiliana na dokta wake kanumba akafika
nyumbani na kumfanyia vipimo ikagundulika amefariki dunia lakini dokta
hakumuambia mdogo ake kanumba mpaka alipopelekwa muhimbili ikabainika
amefariki dunia kutokana na uvimbe ndani ya ubongo.Mshitakiwa alikamatwa
Bamaga na kupelekwa kituo cha Polisi cha osterbay.Baada ya kusomewa
mashitaka hayo mshitakiwa alikana .Upande wa jamhuri chini ya wakili
mwandamizi Monica Mbogo umewasilisha ripoti ya kitabibu na ramani ya
tukio pia kutakua na mashahidi watano Setty Bosco,Dr Palpas
Kageiya,Esther Zefania na E.6056 Lenatus.Upande wa mshtakiwa wakili
Peter Kibatala alisema mashahidi wako watano hakuwataja majina.
Hata
hivyo jaji Rose Temba aliyekua anaisikiliza kesi hiyo amehairisha kesi
mpaka itakapopangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa rasmi pande zote mbili
jamhuri na mshitakiwa watajurishwa.
No comments:
Post a Comment