
Mtandao wa dailystar.co.uk wa nchini Uingereza ambao ni maarufu kwa
habari za kidaku, leo hii umechapisha habari ilizodaiwa na mwandishi wa
habari Mfaransa Paschal Rostain kuwa gazeti linaloheshimika nchini
Marekani la Washinton Post linatarajiwa kuandika habari kuwa the most
powerful man in the world, Rais wa Amerika Bw Barack Obama ana mahusiano
ya kimapenzi na mwimbaji Byonce Knowles ambaye ni mke wa mwanamuziki
Jay-Z. Rostain alikaririwa akisema "Unajua katika siku hizi kuna habari
kubwa inatarajiwa kuchapishwa na gazeti la Washington Post kuwa Obama na
Beyonce wana uhusiano usiofaa, na akaongeza "Dunia nzima italiongelea
hili sana"
Lakini msemaji wa gazeti hilo Wasington Post Bw Kriss Corattialipoulizwa
juu ya habari hiyo akasema hana habari yeyote juu ya hilo ila akaongeza
Rais Obama na mkewe wamekuwa na matatizo hivi karibuni, "Lakini sijui
zaidi ya hapo"
Baada ya yote hayo Paschal Rostain sasa ameeleza kuwa hajawahi kusema kitu chochote ya Rais Obama na mkewe.
Beyonce kupitia msemaji wake alikanusha madai hayo na kusema "Ni
kichekesho". Hata hivyo inafahamika kuwa familia ya Obama ni rafiki na
familia ya Beyonce Knowles ambapo Beyonce aliimba siku ya kuapishwa
Barack Obama na vile vile aliimba katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa
ya Michelle Obama kutimiza miaka 50.

Ahsante sana kwa wimbo mzuri. Obama akimshukuru Beyonce siku ya kuapishwa kwake.

Siku ya kuapishwa Obama

Happily married; Beyonce na mumewe Jay-Z
No comments:
Post a Comment