Wabunge
nchini wamesema habari ya Gazeti la Uingereza la Daily Mail on Sunday
kuwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete inafumbia macho ujangili ni
upotoshaji na serikali inapaswa kumtaka mwandishi huyo aombe radhi.
Pia wamesema habari hiyo kutolewa haraka bila kuulizwa upande wa pili
–serikali ya Tanzania - huku kukiwa na kikao kuhusu masuala hayo nchini
humo ni mwendelezo wa vyombo vya Magharibi kutozitakia heri nchi
changa.
Umoja wa Wabunge Unaoshughulikia Hifadhi ya Wanyamapori na Mazingira
nchini, ulieleza hayo jana katika taarifa yake kwa waandishi wa habari
kuwa gazeti hilo halijui kinachotokea nchini dhidi ya ujangili wa tembo
na faru.
Katibu wa Umoja huo, Mbunge wa Dole, Sylvester Mabumba alisema
kutokana na habari hiyo mkutano wa leo unaohusu uhifadhi wa viumbe hai
unaofanyika Uingereza unamvua nguo Rais, kwani habari ile ilidai kuwa
kuwa mikono yake inanuka damu ya tembo na faru kwa nia ya kupata fedha
za uchaguzi wa mwakani.
“Jambo la kujiuliza ni kwa nini habari hii itoke haraka kiasi hiki
kabla ya mkutano wa kesho (leo), huu ni udhalilishaji na tunaiomba
Serikali imtake mwandishi aombe radhi kwani alichoandika si cha kweli na
pengine ana ajenda ya siri,” alisema Mabumba.
Pia alizungumzia suala la Waziri Kivuli wa Maliasili, Peter Msigwa
(Chadema) kukaririwa na gazeti hilo akisema Serikali haifanyi kitu
katika kukabiliana na ujangili. Mabumba alisema kitendo cha mbunge huyo
kinadhihirisha asivyo Mzalendo kwa nchi yake.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo wenye wajumbe zaidi ya 20, Mbunge wa
Igalula, Athuman Mfutakamba, alisema watajadiliana na Bunge ili kutoa
azimio la pamoja kuhusu habari hiyo.
Alisema ni ukweli kuwa biashara hii haramu ya ujangili wa tembo na
faru inafanywa na mataifa makubwa, huku Rais akiwa mstari wa mbele
kuipinga hata akaidhinisha Operesheni Tokomeza Ujangili.
“Umoja wetu umeshtushwa na taarifa za gazeti hili, kwani Rais
aliagiza faru kutoka nje ili waendelee kuvutia watalii na kuchangia pato
la Taifa ambalo kwa mwaka huiingizia Tanzania fedha nyingi za kigeni,”
alisema.
Mfutakamba alisema kutokana na juhudi za Rais Kikwete kutumia vyombo
vya usalama, mwaka jana kuna kesi 322 mahakamani huku zikikamatwa tani
12 za meno ya tembo.
Katika Daily Mail on Sunday la Februari 8-9 mwandishi Martin Fretcher
alihoji kama itakuwa halali kwa Mwana Mfalme Prince William na Waziri
Mkuu wa Uingereza, David Cameron kupeana mikono na Rais Kikwete kwenye
mkutano huo wa kimataifa unaoanza leo, Lancaster House jijini London.
Mwandishi huyo alionesha kutoridhishwa na Rais Kikwete kupewa
mapokezi makubwa katika kikao hicho cha kudhibiti ujangili kwa kuweka
mikakati ya kuwinda wanyamapori hasa tembo na faru wasiangamie kutokana
na vitendo vya ujangili.
Katika mwendelezo wa kupotosha, alidai kwamba Kikwete hana juhudi wala mikakati ya kulinda wanyama hao

No comments:
Post a Comment