BUNGE LAKANUSHA TUHUMA ZA PAUL MAKONDA KUHUSIKA NA WIZI WA SIMU BUNGENI.
Kitengo
cha ulinzi na usalama cha Bunge kimetoa taarifa ya kukanusha, tuhuma
zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zikimhusisha Mbunge wa Bunge
maalumu la Katiba ndugu Paul Makonda kuhusika na wizi wa simu ya Mjumbe
wa Bunge la
Katiba.
Akitoa taarifa hiyo mbele ya Bunge maalumu
la katiba, Mwenyekiti wa muda wa Bunge maalumu, Mh. Pandu Amiri Kificho
alisema;"Waheshimiwa wabunge taarifa inasomeka kama ifutavyo; Taarifa
ya upotoshaji zilizotolewa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Mh. Paul
Makonda, anahojiwa na vyombo vya usalama vya Bunge kwa tuhuma za wizi wa
simu.
(Sasa Kitengo cha usalama chetu ambacho hicho
kinachotegemewa ndiyo kinamuhoji, kinatoa taarifa hii,ili kuweka wazi na
kuondoa hiyo tuhuma ya upotoshaji iliyotolewa) Mnamo tarehe 27/02/2014
kwenye vyombo vya habari hususani kwenye
mitandao ya kijamii,
zilitolewa taarifa kwamba Mh. Paul Makonda anashikiliwa na vyombo vya
usalama vya Bunge kwa mahojiano kutokana na tuhuma za wizi wa simu ya
mjumbe mwenzake ndani ya ukumbi wa Bunge.
Mtoa taarifa kwenye
mitandao hiyo alieleza kwamba, wakati anatoa taarifa yake Mh. Paul
Makonda, alikuwa chini ya ulinzi akipekuliwa na kuhojiwa kwa tuhuma za
wizi huo. Kitengo chetu kinasema ukweli ni kwamba, taarifa hiyo ni ya
uongo (makofi) na yenye nia ya kumchafua Mh. Paul Makonda (makofi)
pamoja na taswira mzima ya Bunge Maalumu.
Mh. Paul Makonda ambaye
ni mjumbe wa Bunge hili maalumu hana tuhuma yeyote inayohusiana na wizi
wa kitu (makofi) chochote ndani ya maeneo ya Bunge hili maalumu, tangu
ajisajiri kama mjumbe wa Bunge hili maalumu na wala hajawahi kupekuliwa
na kutuhumiwa (makofi) kwa kosa lolote la aina hiyo na hivyo hashikiliwi
wala haojiwi na chombo chochote cha
usalama wa Bunge (makofi).
Waheshimiwa
wabunge naomba niendelee kukemea, kwa mambo ya namna hii, ambayo
yanachafua Mjumbe mmoja mmoja na hatimaye kuchafua Bunge hili maalumu
lenye heshima kubwa (makofi).
Tuwaombe wote wenye mitandao ya kijamii, lakini na vyombo vingine vya habari vyote tuache mtindo huu. Tuache mtindo
huu,
ni mambo ambayo yanaweza kumpa nafasi yule, ambaye anazuliwa kwa tuhuma
za uongo wa aina hiyo, hata kuweza kufungua mashtaka akiona inafaa
(makofi).
Hii ni kwa yule atakayekuwa ametuhumiwa, lakini bado
kwa kutuhumiwa mjumbe mmoja wapo, kwa taarifa za uongo za aina hii, hii
inachafua heshima ya Bunge hili (makofi).
Kwa hiyo, niiombe
mitandao hiyo ya kijamii, niombe vyombo vya habari, Televisheni na Radio
hata wale wanaoandika kwenye magazeti mbalimbali kwamba jambo hili
hatutaki litokee kwa mara nyingine tena (makofi). Tujitahidi sana, tuwe
tunatoa taarifa zenye ukweli ambazo zitakua na maana kwa jamii yetu ya Tanzania.
Jambo
hili tuachane nalo, halifai, lisituchanganye na kutuvunjia heshima zetu
wajumbe lakini pia Bunge hili maalumu tukufu. Nawashukuru sana kwa
hilo"
No comments:
Post a Comment