Ni wakati ambapo Wakristo wanakumbushwa kutubu dhambi, kuwa sisi ni mavumbi na mavubini tutarudi, hii inatufanya tujione kwamba mwili tulionao si kitu cha kujivunia kwa kuwa siku si nyingi utakuwa tena mavumbi, bali tukaze mwendo kuzilinda roho zetu ambazo baada ya kutoka katika mwili huu wa nyama zitaishi milele mbinguni. Mfungo wa Kwaresma unawaalika wakristo kujinyima kwa ajili ya wale ambao hawana kitu. Tofauti ya mfungo wa Kwaresma na mifungo mingine ni kwamba, katika mfungo wa Kwaresma, tunafanya mazoezi ya Kiroho, kutubu dhambi zetu, kujikatalia mambo mbalimbali ya kimwili kama chakula na mavazi. Kile tunachojikatalia tunatakiwa tukikusanya na kuwapa wale ambao wana uhitaji. Kwa mfano, kujikatalia labda kula nyama kwa kipindi chote cha mfungo wa kwaresma kwa familia, kutafanya labda kusevu pengine shilingi 100,000/= hiyo laki moja ninatakiwa niwape maskini moja kwa moja au kupitia kwa mashirika kama vituo vya watoto Yatima........ Sio wakati wa kufunga kwa lengo la kukata wait kama tunavotania lakini kufunga hii iambatane na matendo ya huruma. Kuwatembeela wafungwa na kuwapelekea nguo, kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, kuwapa lifti wanafunzi wanaochelewa mashuleni kila siku na kunyeshewa mvua, kuhudhuria ibada mbalimbali mara kwa mara.
Huu ni wajibu wa Wakristo wakati wote, ila wakati huu wa mfungo wa Kwaresma tunakumbushwa na kuimarishwa kwa ukaribu zaidi pale tulipoegea kuwa wema.
Goldentz inawatakia Wakristo wote Mfungo mwema na wenye neema na baraka tele
No comments:
Post a Comment