Tukio
hilo lililoacha maswali mengi lakini majibu kiduchu huku jeshi la
polisi likihaha kuwanasa wauaji, lilijiri Machi 20, mwaka huu nyumbani
kwake, Kitunda -Machimbo, Ilala jijini Dar es Salaam.
MAZINGIRA YA KUUAWA
Kwa
mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka Jeshi la Magereza, Ukonga, Dar
alikokuwa anafanyia kazi mpaka kifo chake, huenda marehemu alitekwa
kwanza, kisha akateswa na baadaye kuuawa kikatili.
“Ukiangalia
mazingira yanaonesha bosi (marehemu) alitekwa kwanza, akateswa sana na
baadaye kuuawa,” kilisema chanzo hicho huku kikiangua kilio cha utu
uzima.
MWILI WAKUTWA CHOONI
Habari zaidi zinadai kuwa baada ya kumuua, watu hao waliuburuza mwili hadi kwenye choo cha nje ambako waliutupa ndani yake.
Wengine
walipingana na kauli hiyo, wakisema kuwa huenda afande huyo alipotekwa
aliteswa kwanza kisha akaburuzwa hadi chooni akiwa hajiwezi ambako
aliuawa.
“Mimi
napingana na madai kwamba aliuawa kisha mwili wakautupa chooni kwa
sababu, mwili ulikutwa chooni ndiyo lakini pembeni yake kulikuwa na
vipande viwili vya matofali ambavyo huenda vilitumika kumpigia marehemu
hadi kufa, maana mwili wake ulikutwa na jeraha usoni,” kilisema chanzo
kingine.
KUNYONGWA KWATAJWA
Taarifa
zingine zilidai kuwa marehemu ni kama alinyongwa kwanza kisha kupigwa
na tofali hali iliyosababisha kifo chake cha kimyakimya bila kupiga
kelele kwa vile matofali yaliyokutwa chooni hayakuwa na ukubwa wa
kutumika kumpigia mtu hadi kufa.
SAA CHACHE KABLA YA KIFO
Vyanzo
vingine vya habari vilisema kwamba siku ya tukio, marehemu alipotoka
kazini alipitia dukani na kununua soda mbili ambazo polisi walizikuta
mezani sebuleni zikiwa zimenywewa nusu.
MKEWE AHUSISHWA, AKAMATWA, KWA NINI?
Habari zaidi zilisema kwamba marehemu Nkuba alikuwa akiishi na mkewe, Cheula tu kwani watoto wao walikuwa masomoni.
Inasemekana
kwamba marehemu alikuwa na mazoea ya kutangulia kufika nyumbani kabla
ya mke wake kwa vile mwanamke huyo anafanya biashara ya kuuza chakula
Ukonga-Mazizini, Dar na hurudi nyumbani usiku mwingi.
Ikadaiwa kuwa siku ya tukio, mwanamke huyo aliwahi kurudi akiwa amepanda bodaboda.
“Mkewe
ambaye ni mdogo, maana alimuoa baada ya mke mkubwa kufariki dunia,
alipokaribia kwake na bodaboda inadaiwa alimwambia dereva kuwa asifike
nyumbani kabisa kwa vile hali si shwari.
“Tunasikia kwamba aliposhuka alikwenda mwenyewe nyumbani kwake na kukuta mlango uko wazi. Akaingiwa na hofu.
“Basi,
akaenda baa ya jirani na kuwaambia anaowajua kwamba amefika nyumbani na
kukuta mlango uko wazi na kila akiipiga simu ya mumewe, haipatikani.
“Ndipo
majirani hao na mwanamke huyo wakaenda nyumbani hapo na kuingia.
hawakukuta mtu, hata walipoita Nkuba, Nkuba, wapi! Kimya!
“Walikwenda
uani ambako walikuta alama za mburuziko wa kitu, wakazifuata hadi
chooni ambako waliukuta mwili wa kigogo huyo akiwa ameshafariki dunia na
ndipo polisi walipopewa taarifa.
“Mwili wake ulipelekwa Hospitali ya Amana, baadaye wakauhamishia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,” kilisema chanzo.
Polisi walipofika, habari zinadai kuwa walimkamata mwanamke huyo kutokana na mazingira yenye utata.
“Tunasikia
polisi walishangaa kama yeye ndiyo mwenye nyumba iweje akute mlango
wazi ahofie kuingia wakati wanaishi wawili tu? Kwa nini asiingie na
kumuita mumewe, pengine alipitiwa na usingizi?
“Halafu
kingine, ni kwa nini alimwambia dereva wa bodaboda asimfikishe
nyumbani hali si shwari? Ni hali gani hiyo ambayo haikuwa shwari wakati
alikuwa hajaingia ndani?” kilihoji chanzo hicho.
Kwa cheo cha marehemu, angekuwa JWTZ nafasi yake ni meja, kwa jeshi la polisi angekuwa kamanda wa polisi wa wilaya (OCD).
Mwili
wa marehemu Nkuba ulisafirishwa Machi 22, mwaka huu kupelekwa Shinyanga
kwa mazishi. Ameacha watoto wanne. Mungu ailaze pema peponi roho yake.
Amina.
NA GPL
No comments:
Post a Comment