Mashabiki
wa Manchester United waliojawa hasira jana usiku walimgeuka kocha wao
wa zamani Sir Alex Ferguson baada ya kushuhudia timu yao ikiadhibiwa na
mahasimu wao Manchester City katika uwanja wao wa nyumbani Old
Trafford usiku wa jana.
Vijana wa Manuel Pellegrini waliwatandika United 3-0 kupitia magoli
ya Yaya Toure na Eden Dzeko na kuzidi kuwaondolea vijana wa Moyes kupata
hata nafasi ya kushiriki michuano ya ulaya msimu ujao.
Na mashabiki wa United wakaamua kuhamishia hasira zao kwa Ferguson, ambaye ndio aliyemteua Moyes kumrithi nafasi yake.
Ferguson ambaye alikuwa jukwaani akitazama mchezo alikuwa akitupiwa maneno ya kejeli kuhusu uamuzi wake wa kumkabidhi timu Moyes wakati Moyes alikuwa akitukanwa kabisa na mashabiki kadhaa waliokuwa wamekaa karibu yake.
Hali ilizidi kuwa tata baada ya mashabiki kutaka kulishusha bango
liliopo katika jukwaa la Stretford End ambalo limeandikwa ujumbe
unaosomeka ‘Chosen One’ huku kukiwa na picha ya Moyes – hata hivyo
polisi wa kulinda amani uwanjani walifanikiwa kuzima jaribio la
mashabiki kulishusha bango hilo.
No comments:
Post a Comment