Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa
Bunge hilo mjini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa Sura ya Kwanza na Sita
wa rasimu ya Katiba mpya.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati namba tano Assumpter Mshama akiwasilisha maoni ya
wajumbe wa Kamati yake mjini Dodoma juu ya uchambuzi wa sura ya kwanza
na sita ya wa rasimu ya Katiba mpya.
Baadhi
ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwasili kwenye ukumbi wa Bunge
mjini Dodoma kwa ajili ya kusilikiliza uwasilishaji wa sura ya kwanza
na sita ya rasimu ya Katiba mpya.Picha na Bunge Maalum la Katiba.
Na Magreth Kinabo- Dodoma
Baadhi
ya Kamati 12 za Bunge Maalum la Katiba leo zimeanza kuwasilisha taarifa
zao kuhusu sura ya kwanza nay a sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Bunge hilo, mjini Dodoma, huku maoni ya
walio wengi wapendekeza Serikali Mbili.
Uwasilishaji
wa taarifa hizo ulianza mapema asubuhi mara baada ya Mwenyekiti wa
Bunge hilo, Samuel Sitta kuanza kikao, ambapo Kamati mbili ndizo
zilizopata fursa ya kuwasilisha, kwa mujibu wa muda uliopangwa .Kamati
nyingine zitaendelea sasa 10: 00 jioni.
Kamati
iliyokuwa ya kwanza kuwasilisha taarifa hiyo ni Kamati namba mbili,
ambayo Mwenyekiti wake ni Shamsi Vuai Nahodha , ambaye ndiye
aliyeiwasilisha katika Bunge hilo.
Akiwasilisha
taarifa hiyo, Nahodha, aliliarifu Bunge hilo, kuwa zipo baadhi ya ibara
ambazo hakikuungwa mkono kwa theluthi mbili kwa mujibu wa Kanuni ya
64(1) ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba za mwaka 2014.
Alizitaja
ibara hizo ni ibara ya inayohusu “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”,
ibara inayohusu “Ukuu na Utii kwa Katiba,” ibara ya 60 inayohusu “Muundo
wa Muungano “na ibara ya 61 inayohusu” Vyombo vya Utendaji vya Jamhuri
ya Muungano”.
"Kutokana
na hali hiyo na kwa kuzingatia kanuni niliyoitaja hapo awali, ibara
hizi zinachukuliwa kuwa zimefanyiwa maamuzi, lakini hazikupata theluthi
mbili ya upande mmoja. Kwa msingi huo Kamati yangu inazileta ibara hizo
pamoja na ibara nyingine mbele ya Bunge hili Maalum ili kufanyiwa
maamuzi ya pamoja,” alisema Nahodha.
Akiwakilisha
maoni ya walio wengi kuhusu sura ya kwanza ibara ya kwanza(i)inayohusu
“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” alisema wajumbe walikuwa na mjadala
maana na maneno ya “Muungano na “Shirikisho”. Hata hivyo katika mjadala
huo ufafanuzi kina ulitolewa kuhusu maneno hayo.
Alisema
neno Muungano ni makubaliano ya zaidi ya nchi moja kuunda dola moja
yenye nguvu ambapo majukumu ya msingi ya nchi hizo yanakabidhiwa kwenye
Serikali ya Muungano, wakati Shirikisho ni makubaliano ya nchi mbili au
zaidi zinazounda Serikali moja chini ya kiongozi mmoja.
Hivyo
baada ya ufafanuzi huo wajumbe walifanya maamuzi katika ibara ya
kwanza(1)wajumbe wengi walipendekeza neno shirikisho lifutwe kwa sababu
tatu, ambazo kwanza ni hati ya makubaliano ya Muungano inazungumzia
kuwepo kwa Serikali mbili yaani Serikali ya Muungano na Serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar. Hata Rasimu ya Katiba ibara 1(3) inatambua hati
ya Muungano kama msingi na muendelezo wa makubaliano hayo.
Pili
hati hiyo ya Muungano mpaka sasa bado haijafutwa na wala
haijabadilishwa na tatu Shrikisho la serikali tatu linalopendekezwa
katika rasimu , litakuwa dhaifu kiasi cha kushindwa kudhibiti ulinzi wa
eneo la bahari ya Hindi lenye rasilimali nyingi ambazo mataifa makubwa
wanaziwania.
Aliongeza
kuwa udhaifu huo utayapa mwanya mataifa hayo kuzirubuni nchi washirika
zisichangie gharama za kuendesha Serikali ya Shirikisho, hasa kwa
kuzingatia kuwa Serikali Shirikisho haina vyanzo vya uhakika vya mapato
,hivy endapo jambo hilo likitokea Shirikisho litadhoofika na hatimaye
kuvujika.
Aliongeza
kuwa katika sura ya sita ibaraya 60 kuhusu Muundo wa Jamhuri ta
Muungano wajumbe wengi walikubaliana kuwa Muundo wa Serikali Mbili kama
ilivyoanishwa katika hati ya Muungano wa Tanzania, baada ya kupiga kura
kwa ajili ya kupata uamuzi ,theluthi mbili upande wa Tanzania Bara
haikupatikana.
Hata
hivyo wajumbe wengi walipendekeza ibara hiyo ifanyiwe marekebisho kuwa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na Serikali mbili ambazo ni
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar.
Nahodha
alisema kwa maoni ya watu wachache , katika sura ya kwanza 1(1)
walipendekeza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili limetokana na Muungano wa Nchi huru mbili za Jamhuri ya
Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Aidha
aliongeza kuwa katika sura ya sita, ibara, 60 hadi 69 zinahusu Muundo
wa Serikali walipendekeza zibaki na zisomeke kama zilivyo katika rasimu.
Kwa
upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba tano (5)ya Bunge hilo,
Assumpter Mshama ambayo ilikuwa ya pili kuwasilisha ripoti yake ,
alisema ibara ya kwanza(1) haikupata theluthi mbili ya wajumbe wote
kutoka Tanzania Bara,lakini ilipata theluthi mbili ya wajumbe kutoka
Zanzibar.
Aliongeza kuwa ibara ndogo ya (2) na (3) zilipata theluthi mbili ya wajumbe wote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Hivyo
wajumbe walio wengi kwa kuzingatia Hati ya Makubaliano walipendekeza
mfumo wa Serikali Mbili ndiyo unaofaa, ndiyo utakaoimarisha Muungano
kama changamoto zilizobainishwa zitatuliwa kisheria na kikatiba.
Assumpter
alisema katika sura sita ibara ya 60 ilikataliwa na theluthi mbili ya
wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Hivyo walipendekeza ibara ya
60 (1) itakuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa
Serikali mbili, ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema
maoni ya walio wachache sura ya kwanza ibara ndogo ya kwanza wajumbe
walipendekeza kuwa ibaki kama ilivyo lakini irekebishwe kidogo, isomeke
Shirikisho la Jamhuri ya Tanzania, ni Shirikisho ambalo limetokana na
Muungano wa Nchi mbili za Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
ibara 1(4) Nchi nyingine yoyote ya Afrika itaweza kujiunga na Shirikisho ili mradi tu inakubaliana na masharti ya Katiba hii.”
Alisema
sababu walizozitaja ni Muungano wa Tanzania umetokana na Jamhuri ya
mbili kuungana kwa hiari, jina la awali lililotajwa katika Mkataba wa
Muungano lilikuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tangayika na Zanzibar.Jina
hili lilibailishwa na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika taarifa za kamati hizo, baadhi ya ibara zilifanyiwa marekebisho na nyingine zibaki kama zilivyo.
No comments:
Post a Comment