Mhubiri
mtata wa kiisilamu nchini Kenya Abubakar Shariff anayejulikana kwa jina
maarufu Makaburi ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana mjini
Mombasa. Polisi wamethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema
aliuawa na akiwa mtu mwingine aliyefahamika kama Bahero.
Makaburi aliuawa nje ya gereza la Shomi la Tewa mjini Mombasa.
Marehemu Shariff alikuwa anafikishwa mahakamani mara kwa mara kwa tuhuma
za kuhusika na vitendo vya kigaidi. Habari zinasema hali ya tahadhari
imeanza kushuhudiwa Mombasa ambapo vijana wameanza kujikusanya kwa ajili
ya kufanya vurugu.
Kuuawa kwa Makaburi kumetokea miaka miwili baada ya mshirika wake
Aboud Rogo kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa
akimpeleka mkewe hospitali mjini Mombasa, tukio ambalo lilisababisha
maandamano ya siku tatu mjini humo.
No comments:
Post a Comment