ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Saturday, April 19, 2014

WHAT A FAITH! Wakristo Wakatoliki Parokia ya mwenge wakishiriki katika ibada ya Ijumaa kuu licha ya mvua kubwa sana kunyesha.



Katika hali isiyokuwa ya kawaida, waumini wa Kikatoliki walishiriki kwa utulivu mkubwa kabisa katika ibada ya Ijumaa Kuu, katika kukumbuka mateso na kifo cha Yesu Kristo. Kilichonifanya nione kwamba imani ipo tena kubwa, ni pale wakristo hao bila kujali mvua kubwa iliyoanza kunyesha wakati uleule wa kuanza kuabudu msalaba. Lakini bila kujali waliendelea kukaa katika misururu mirefu huku wengine wakiwa na watoto wao wadogo na kuhakikisha kila mmoja amepata nafasi ya kuubusu msalaba na hali kadhalika wakati wa Komunio. Sikutarajia watu hasa vijana na wasichana warembo waliokuwa wameshaseti nywele zao kwa ajili ya Pasaka kukubali kunyeshewa mvua kiasi kile. Ingekuwa harusi, au sherehehe, au hata mazishi, watu huwa wanasepa kwanza kupisha mvua ipite. SIvyo ilivyokuwa katika ibada hii ya Ijumaa kuu. Ndiyo maana nikajenga dhana kwamba, imani bado ipo aisee. Labda ni kwa Ijumaa Kuu tu?

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...