Balozi wa Malawi nchini Tanzania Mhe.
Flossy Gomile-Chidyaonga (pichani) amefariki dunia jana jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.

“Ni
kwa masikitiko makubwa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa (ya Malawi) unauarifu umma kufariki dunia kwa Balozi Flossy
Gomile-Chidyaonga baada ya kuugua kwa muda mfupi jijini Dar es salaam mchana huu”, imesema taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara hiyo Quent Kalichero.

“Tangu mwaka 2006 Marehemu Bi Flossy Gomile-Chidyaonga alikuwa
Naibu Balozi wa Malawi London kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania mnamo Septemba mwaka 2011”, imesema taarifa hiyo na kuongezea kuwa taratibu za mazishi zitatangazwa baada ya taratibu kukamilika.

No comments:
Post a Comment