Simanzi
kubwa imetanda katika Kijiji cha Roo, Kata ya Masama Mashariki wilayani
Hai, Kilimanjaro, baada ya kijana mwenye umri wa miaka 32 kuwaua wazazi
wake wawili kwa kutumia panga na shoka, kisha kuchoma moto nyumba yao.Kijana
huyo aliyetambulika kwa jina la Yusuph Njau aliwaua wazazi wake,
Shahidu Njau (60) na Minae Swai (57) baada ya kuwafungia ndani na
kuwakata kata kwa kutumia shoka na panga.Akizungumza na mwandishi,
Diwani wa Kata ya Masama Mashariki, Ally Mwanga alisema mauaji hayo
yalitokea juzi majira ya saa 12: 30 jioni, katika nyumba waliyokuwa
wanaishi wanafamilia hao.
Mwanga
alisema baada ya kijana huyo kufanya mauaji hayo, alichukua uamuzi wa
kuchoma nyumba huku miili ya wazazi wake ikiwa ndani, ambapo majirani
walitoa msaada wa kudhibiti moto huo baada ya kuona moshi ukifuka ndani.
Alisema
wakati wananchi wakiendelea kuudhibiti moto huo, ndipo waliona miili ya
marehemu ikiwa inavuja damu, hali iliyosababisha kutoa taarifa Polisi.
Alisema
mtuhumiwa alitoroka baada ya matukio hayo na kwamba maziko ya wazazi
wake yalitarajiwa kufanyika jana jioni kijijini kwao Roo.
Mwanga
alisema taarifa za awali zilizopatikana kuhusiana na tukio hilo kuwa
chanzo ni matumizi ya dawa za kulevya na bangi ambazo amekuwa akitumia
kwa muda mrefu kijana huyo.
“Hili
tukio ni la kutisha sana, linahuzunisha sana, kijana huyu amekuwa
akitumia dawa za kulevya kwa muda mrefu, hivyo kichwa kimeathiriwa kwa
matumizi hayo,” alisema Mwanga.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Roo, Khalfan Swai, alilieleza kuwa
kijana huyo amekuwa na matukio ya kutishia watu hapo kijijini, na
amewahi kufungwa kwa muda baada ya kuwapiga baba mdogo na shangazi yake.
Swai
alisema kijana huyo amekuwa akitembea na shoka na panga kwa kuwatishia
watu, lakini wazazi wake walikuwa wakimtetea kuwa mwana wao hahusiki na
vurugu zozote za kutishia watu.
Pia
alisema kijana huyo awali alikuwa anaishi Dar es Salaam akiwa
anajifunza ngumi za kulipwa, lakini baada ya kuathirika na matumizi ya
dawa za kulevya ndipo aliporejea kijijini.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz akitoa
taarifa
za tukio hilo, alisema Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa
kumtafuta mtuhumiwa, ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
VIA MZALENDO
No comments:
Post a Comment