Serikali
na wapiganaji wa Sudan Kusini wamelaumiana kwa kuvunja makubaliano ya
kusitisha mapigano - masaa tu baada ya makubaliano kufikiwa.
Msemaji
wa jeshi la serikali, Kanali Philip Aguer, alisema wapiganaji
wameshambulia maeneo ya serikali katika mji wa Bentiu leo alfajiri.
Wapiganaji wamewashutumu wanajeshi wa serikali kuwa waliwashambulia katika sehemu kadha katika majimbo ya Upper Nile na Unity.
Makubaliano
ya kusitisha mapigano yalitiwa saini Ijumaa, na yalikusudiwa kumaliza
vita vya miezi mitano ambavyo vimeuwa maelfu ya watu na kulazimisha
zaidi ya milioni moja kuhama makwao.
No comments:
Post a Comment