SIKU moja
baada ya mmoja kati mawaziri wanaotajwa kuwa mizigo, Christopher Chiza,
kupata wakati mgumu kupitisha bajeti ya wizara yake ya Kilimo, Chakula
na Ushirika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoundwa na wabunge
wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), imepania kukwamisha
bajeti ya Wizara ya Maji, inayoongozwa na waziri mwingine mzigo, Profesa
Jumanne Maghembe.Msimamo wa kukwamisha bajeti ya wizara hiyo
ulitangazwa jana na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA).Alisema
mwaka wa fedha 2013/14 unaomalizika Julai 30, serikali iliongeza bajeti
ya Wizara ya Maji kufikia sh bilioni 184, lakini fedha zilizotolewa ni
sh bilioni 86 tu na sh bilioni 98 hazijatolewa hadi sasa, hivyo
kukwamisha miradi mingi ya maji nchini.“Kwa hali hiyo hakuna sababu
yoyote ya kujadili bajeti ya maji ya mwaka 2014/15, kwani bajeti ya
mwaka uliopita hajatekelezwa pamoja na viongozi wa serikali kutumia
Bunge kuwadanganya wananchi, kwamba suala la maji katika maeneo
mbalimbali nchini, likiwemo Jiji la Dar es Salaam litakuwa historia,”
alisema MnyiBBBBBBBBBBBBB
Aliongeza:
“Kwa kuwa tayari randama iliwasilishwa mezani na haikuwafikia wabunge
wote kwa wakati, mimi nimeipata na nimeisoma kwa makini na nimegundua
kwamba miradi mingi ya maji haijatekelezwa licha ya kuwepo mpango mzuri
wa vijiji 10 kila wilaya kupatiwa maji, lakini bado hata miradi hiyo
haijatekelezwa hadi sasa.
“Jambo
hili ni zito kuliko jambo lolote kwani inaonyesha wazi kuwa tatizo la
maji kwa Watanzania halina ufumbuzi, hivyo hakuna sababu ya kujadili
hotuba hiyo na badala yake inatakiwa irudishwe, ili ipitiwe upya na
kamati na hapo ndipo itaweza kujadiliwa.”
Mnyika
alisena anakusudia kumwandikia barua Waziri Magembe, ili asisome bajeti
yake leo kwa madai kuwa miradi mingi ya maji iliyopangwa katika bajeti
ya mwaka wa fedha 2013/2014 hajatekelezwa na mingine haijaanza kabisa.
Mbunge
huyo ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, alienda mbali kwa
kumtaka Maghembe pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na
Uratibu), Stephen Wassira, kuwajibika kwa kujiuzulu kwa kutumia Bunge
kuwadanganya wananchi juu ya mpango mkubwa wa maji katika maeneo mengi
nchini.
Mnyika
alisema kuwa analazimika kufanya hivyo kutokana na bajeti yake kuwa na
mapungufu mengi ambayo hayatoi ufumbuzi kwa Watanzania juu ya tatizo la
maji, hususani katika Jiji la Dar es Salaam.
Mbali na
hilo, alisema hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji ya mwaka huu wa fedha,
ina upungufu mkubwa kutokana na kile alichoeleza kuwa ni uongo wa
mawaziri wa wizara hiyo ambao waliwapa matumaini makubwa Watanzania.
Alisema
serikali haina dhamira ya kweli katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo la
maji na badala yake wamekuwa wakitumia shida za Watanzania kufanya siasa
ambazo hazina matokeo na mipango ya kimaendeleo.
Kwa
mujibu wa Mnyika, kama Waziri Maghembe atalazimisha kuisoma bajeti hiyo,
atamjulisha Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa ushirikiano
wa Baraza la Mawaziri Kivuli la UKAWA, kupanga mikakati ya kukwamisha
bajeti hiyo.
Alisema
katika hatua hiyo Waziri Mkuu Mizengo Pinda ndiye analazimika kutoa hoja
ya kuondoa bajeti ya Wizara ya Maji isijadiliwe na asipofanya hivyo,
naye atatakiwa kuchukuliwa hatua kali.
“Suala la
maji siyo kwa Jiji la Dar es Salaam tu, ili ni janga la kitaifa. Hata
katika vijiji kumi ambavyo viliingizwa katika mpango wa matokeo makubwa
sasa na badala yake mpango huo umegeuka kwa kasi kuwa mpango wa matokeo
mabaya sasa,” alisema Mnyika.
Wakati wa
Bunge la Bajeti la mwaka wa fedha uliopita, Mnyika aliwasilisha hoja
binafsi kuhusu tatizo la maji jijini Dar es Salaam, lakini ilizimwa
bungeni kwa madai kuwa serikali ina mpango wa miradi mikubwa ya maji kwa
nchi nzima.
No comments:
Post a Comment