TUNAOMBA RADHI KWA PICHA INAYOONEKANA KWENYE VIDOKEZO
Mwanafunzi
ambaye amefahamika kwa jina moja la LEMA Alikua akisoma mwaka wa 4 kozi
ya sheria katika chuo kikuu kishiriki cha Mt.Augustino Tawi la Iringa
(Ruaha University College-RUCO).
Taarifa za awali zilizotufikia
zimeeleza kuwamnamo tarehe 24.06.2014 mwanafunzi huyo alikua ametoka
kuangalia michuano ya kombe la dunia na akiwa amelewa akawa anatafuta
chakula cha Usiku na ilikua majira ya saa 5 Usiku, Mwanafunzi huyo
aliingia kwenye mgahawa ambao biashara ilikua imefungwa kwa muda huo
lakini ndani kulikuwapo na Binti ambaye alianza kupiga kelele kwa
kudhani alikua mwizi. Na kwakua eneo hilo mkulikuwa na mlinzi(Mmasai)
ndiye aliyeanza kumshambulia mwanafunzi huyo.
Baada ya tukio hilo wakatokea watu
(2) waliojitambulisha kuwani askari wakaamuru mwanafunzi huyo asipigwe
kwa madai ya kumfikisha kituoni.
Lakini baada ya mwendo mfupi kuelekea
kituoni wananchi wenye hasira kali walimchukua kijana huyo kinguvu na
kwenda kumchoma moto.
Mpaka sasa Kijana huyo amelazwa katika wodi ya watu mahututi (ICU) katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment