Taarifa iliyoanza kusambaa usiku wa July 21 ni kuhusu Mabaki ya miili ya watu ambao wanasemekana zaidi ya 100 kukutwa katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji, kata ya Mbweni, wilaya ya Kinondoni, ikiwa imetelekezwa.
Mabaki hayo ya miili yameonekakana kuvuta mamia ya wananchi waliokuwa
wakishuhudia tukio hilo, baadhi ya mashuhuda walipoulizwa wamesema
mabaki hayo yalikuwa yamehifadhiwa katika mifuko ya plastiki ukiwa
imefungwa juu.
Wameongeza kwa kusema mabaki hayo ambayo yamekaushwa na kuhifadhiwa
katika mifuko ya ujazo wa kilo 25 ni pamoja na miguu, mikono, mbavu na
mafuvu ya vichwa hata hivyo Jeshi la Polisi walifika eneo la tukio na
kuanza kupakia mabaki hayo katika gari lao lenye namba za usajili MS 54
UKH na kuipeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi. (Maelezo na Millard Ayo)
Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi
wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya
kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika
mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji,
Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Sehemu ya mifuko ya plastiki iliyokutwa na viungo hivyo ambavyo
inasemekana ni pamoja na mikono, miguu, ngozi na sehemu nyingine za
miili.
No comments:
Post a Comment