Mkazi
Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma,Bibi
Scholastica Mhagama amesema miaka mingi ameishi maisha dhiki na
kunyanyaswa bila msaada kutoka kwa jamii anayoishi hali ambayo imemfanya
amuombe Mungu amchukuwe ili azikwe kwenye jeneza alilojiandalia.
anasema Scholastica Mhagama (76) mwenye ulemavu wa viungo anayeishi pekee yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi.