Mke wa kigogo (Mugaka),Bi. Leah aliyefanyiwa unyama na
mumewe.
Ilisemekana kwamba ilifika wakati hali ikawa
mbaya kiasi cha baadhi ya majirani kumshauri Mugaka kuachana naye kama anaona
hamfai. Ilisemekana kwamba chanzo cha kufanyiwa unyama huo na kujeruhiwa na
kisu ni madai ya mwanaume huyo kuwa alitumiwa ujumbe mfupi kwenye simu yake,
akiambiwa kuwa mkewe alikuwa akimsaliti kwa kutembea na watu wa nje, wakiwemo
polisi
Kigogo anayetajwa kwa jina moja la Mugaka anayetuhumiwa kumnyanyasa mkewe.
Ilidaiwa
kwamba mkewe alikataa madai hayo na kumtaka mumewe kuitoa namba ya simu
iliyotuma ujumbe huo ili wampigie palepale wakiwa wote, lakini jamaa huyo
alikataa na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili huku akimchoma na kisu
pajani. Jirani wa mtuhumiwa aliyeomba hifadhi ya jina alidai kwamba Mugaka
amekuwa akimpiga, kumtesa, kumdhalilisha mkewe mara kwa mara huku akisikika
kumweleza kuwa ipo siku atamuua
KIGOGO wa shirika moja la kimataifa linalojishughulisha na
watoto yatima, tawi la mkoani Pwani, Tanzania aliyetajwa kwa jina moja la
Mugaka, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 hadi 40, ametupwa rumande
akituhumiwa kumchoma kisu na kumtoa manundu mkewe, Leah (28).Tukio hilo la
kusikitisha lilijiri wilayani Kisarawe, Pwani mwishoni mwa wiki iliyopita. Kwa
mujibu wa habari zilizopatikana, chanzo cha unyama huo kinashangaza huku madai
ya Mugaka ambaye ni afisa mshauri wa shirika hilo yakisema mkewe huyo amekuwa
akimjazia choo kwa kuwa tangu amuoe miaka mitatu iliyopita, ameshindwa kumzalia
mtoto.
Sehemu ya mguu alipochomwa kisu na Bw. Mugaka (mumewe).
Habari ziliendelea
kudai kwamba shirika analofanyia kazi Mugaka linalosimamiwa na mfuko wa rais wa
zamani wa Marekani, Bill Clinton. Madai mazito yalishushwa kwamba Mugaka
amekuwa akimnyanyasa mkewe kwa sababu hiyo, kiasi cha kumtolea maneno ya
kejeli, dharau, kashfa huku akimshushia kipigo ‘hevi’.
Majeraha mengine sehemu ya mguu wa kulia.Kigogo anayetajwa kwa jina moja la Mugaka anayetuhumiwa kumnyanyasa mkewe.
Muonekano wa karibu wa Bi. Leah.
Baba mzazi wa
majeruhi, William Lyima alisema baada ya kupata taarifa za kipigo hicho,
alimpigia simu Mkuu wa Kituo cha
Polisi cha Kisarawe,
OCD Issa na kumtaarifu tukio hilo ambapo askari wake walifika na kuizingira
nyumba ya mtuhumiwa huyo na ilipofika majira ya saa 11:00 alfajiri walifanikiwa
kumtia mbaroni.
Kigogo huyo amefunguliwa mashitaka ya shambulio la kudhuru
mwili na kujeruhi kwa kisu katika jalada lenye kumbukumbu namba
KIS/RB/964/2014-SHAMBULIO LA KUDHURU NA KUJERUHI MWILI akisubiri sheria
kuchukua mkondo wake.





No comments:
Post a Comment